Luke 9:19 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nao wakamjibu, “Wengine wanasema kuwa wewe ni Yohane Mbatizaji; wengine, Elia; wengine, mmojawapo wa manabii wa kale ambaye amefufuka.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakamjibu, “Baadhi husema wewe ni Yahya, wengine husema ni Ilya, na wengine husema kwamba ni mmoja wa manabii wa kale amefufuka.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakamjibu wakisema, Yohana Mbatizaji; lakini wengine, Eliya; na wengine kwamba mmojawapo wa manabii wa kale amefufuka.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakajibu, “Baadhi ya watu wanasema wewe ni Yohana Mbatizaji, wengine wanasema wewe ni Eliya, lakini wengine wanasema wewe ni mmoja wa manabii wa zamani aliyefufuka.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nao wakamjibu, “Wengine wanasema kuwa wewe ni Yohane mbatizaji, wengine wanasema wewe ni Eliya, hali wengine wanasema kuwa wewe ni mmoja wa manabii wa kale ambaye amefufuka.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nao wakamjibu, “Wengine wanasema kuwa wewe ni Yohane Mbatizaji; wengine, Elia; wengine, mmojawapo wa manabii wa kale ambaye amefufuka.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakamjibu, “Wengine husema wewe ni Yohana Mbatizaji, wengine husema ni Eliya na wengine husema, wewe ni mmoja wa nabii wa kale aliyefufuka kutoka kwa wafu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakamjibu, “Baadhi husema wewe ni Yahya, wengine husema ni Ilya, na bado wengine husema kwamba ni mmoja wa manabii wa kale amefufuka kutoka kwa wafu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakamjibu wakisema, Yohana Mbatizaji; lakini wengine, Eliya; na wengine kwamba mmojawapo wa manabii wa kale amefufuka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nao wakamjibu, “Wengine wanasema kuwa wewe ni Yohane Mbatizaji; wengine, Elia; wengine, mmojawapo wa manabii wa kale ambaye amefufuka.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wakajibu wakisema: Wanakusema kuwa u Yohana Mbatizaji, wengine: Elia, wengine husema: Amefufuka mmoja wao wafumbuaji wa kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakamjibu wakisema, Yohana Mbatizaji; lakini wengine, Eliya; na wengine kwamba mmojawapo wa manabii wa kale amefufuka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao wakajibu: “Wamoja wanasema kwamba wewe ni Yoane Mubatizaji, wengine wanasema kwamba wewe ni Elia, na wengine wanasema kwamba wewe ni mumoja wa manabii wa zamani aliyefufuka.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakajibu, wakasema, Yohana Mbatizaji: na wengine, Eliya: na wengine kwamba nabii mmoja katika wale wa kale amefufuka.