Luke 9:22 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akaendelea kusema kwamba ni lazima Mwana wa Mtu apate mateso mengi na kukataliwa na wazee na makuhani wakuu na waalimu wa sheria na kuuawa, lakini siku ya tatu atafufuliwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akasema, “Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi na kukataliwa na wazee, viongozi wa makuhani, na walimu wa Torati, na itampasa auawe, lakini siku ya tatu kufufuliwa kutoka mauti.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi, na kukataliwa na wazee na wakuu wa makuhani na waandishi, na kuuawa na siku ya tatu kufufuka.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akasema, “Ni lazima Mwana wa Adamu apate mateso mengi. Nitakataliwa na viongozi wazee wa Kiyahudi, viongozi wa makuhani na walimu wa sheria. Na nitauawa. Lakini siku ya tatu nitafufuliwa kutoka kwa wafu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Akaendelea kusema: “Ni lazima Mwana wa Mtu apate mateso mengi na kukataliwa na wazee na makuhani wakuu na walimu wa Sheria; atauawa, lakini siku ya tatu atafufuliwa.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akaendelea kusema kwamba ni lazima Mwana wa Mtu apate mateso mengi na kukataliwa na wazee na makuhani wakuu na waalimu wa sheria na kuuawa, lakini siku ya tatu atafufuliwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akasema, “Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi na kukataliwa na wazee, viongozi wa makuhani na walimu wa sheria, naye atauawa na siku ya tatu atafufuka.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akasema, “Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi na kukataliwa na wazee, viongozi wa makuhani, na walimu wa Torati, na itampasa auawe, lakini siku ya tatu kufufuliwa kutoka mauti.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi, na kukataliwa na wazee na wakuu wa makuhani na waandishi, na kuuawa na siku ya tatu kufufuka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akaendelea kusema kwamba ni lazima Mwana wa Mtu apate mateso mengi na kukataliwa na wazee na makuhani wakuu na waalimu wa sheria na kuuawa, lakini siku ya tatu atafufuliwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawaambia: Imempasa Mwana wa mtu kutwa mengi na kukataliwa nao wazee na watambikaji wakuu na waandishi, mpaka auawe, kisha afufuliwe siku ya tatu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi, na kukataliwa na wazee na wakuu wa makuhani na waandishi, na kuuawa na siku ya tatu kufufuka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye akaongeza kuwaambia: “Sherti Mwana wa Mutu ateswe na kukataliwa na wasimamizi wa watu, pamoja na walimu wa Sheria. Atauawa na kwa siku ya tatu kisha kufa kwake, atafufuka.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akawaagiza na kuwaamuru wasimwambie mtu neno hili, akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi na kukataliwa na wazee na makuhani wakuu, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.