Luke 9:24 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana, mtu anayetaka kuyaokoa maisha yake mwenyewe, atayapoteza; lakini anayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, atayaokoa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayaokoa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yeyote miongoni mwenu anayetaka kuyaponya maisha yake atayaangamiza. Lakini yeyote atakayeyatoa maisha yake kwa ajili yangu atayaokoa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana, mtu anayetaka kuyaokoa maisha yake mwenyewe, atayapoteza; lakini atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, atayaokoa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana, mtu anayetaka kuyaokoa maisha yake mwenyewe, atayapoteza; lakini anayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, atayaokoa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana ye yote atakayekuyaponya maisha yake atayapoteza, lakini ye yote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayaokoa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayaokoa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana, mtu anayetaka kuyaokoa maisha yake mwenyewe, atayapoteza; lakini anayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, atayaokoa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maana mtu anayetaka kuiokoa roho yake ataiangamiza. Lakini mtu atakayeiangamiza roho yake kwa ajili yangu mimi, huyo ataiokoa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana mutu anayetaka kulinda uzima wake ataupoteza; lakini yule atakayetoa uzima wake kwa ajili yangu ataulinda.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana mtu akitaka kuisalimisha roho yake ataiangamiza, nae atakae kuitoa roho yake kwa ajili yangu, huyu ataisalimisha.