Luke 9:29 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alipokuwa akisali, sura yake ilibadilika, mavazi yake yakawa meupe na kungaa sana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipokuwa akiomba, sura ya uso wake ikabadilika, nayo mavazi yake yakametameta kama miali ya radi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa katika kusali kwake sura ya uso wake ikageuka, mavazi yake yakawa meupe, yakimeta-meta.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu alipokuwa akiomba, uso wake ulianza kubadilika. Nguo zake zikawa nyeupe, zikang'aa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Alipokuwa akisali, sura yake ilibadilika, mavazi yake yakawa meupe na kung'aa sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alipokuwa akisali, sura yake ilibadilika, mavazi yake yakawa meupe na kung'aa sana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipokuwa akiomba, mwonekano wa sura yake ukabadilika, mavazi yake yakametameta kama mwanga wa umeme wa radi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipokuwa akiomba, sura ya uso wake ikabadilika, nayo mavazi yake yakametameta kama mwanga wa umeme wa radi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa katika kusali kwake sura ya uso wake ikageuka, mavazi yake yakawa meupe, yakimetameta.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alipokuwa akisali, sura yake ilibadilika, mavazi yake yakawa meupe na kungaa sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipokuwa akiomba, sura ya uso wake ikawa nyingine, nazo nguo zake zikawa nyeupe na kumerimeta.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa katika kusali kwake sura ya uso wake ikageuka, mavazi yake yakawa meupe, yakimeta-meta.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye alipokuwa akiomba, sura yake ikageuka, nazo nguo zake zikageuka nyeupe sana na zenye kumetameta.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ikawa alipokuwa akisali, sura ya uso wake ikageuka, na mavazi yake yakawa meupe, yakimetameta.