Luke 9:32 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Petro na wenzake walikuwa wamelemewa na usingizi mzito, hata hivyo waliamka, wakauona utukufu wake, wakawaona na wale watu wawili waliokuwa wamesimama pamoja naye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Petro na wenzake walikuwa wamelala usingizi mzito. Walipoamka, wakaona utukufu wa Isa na wale watu wawili waliokuwa wamesimama pamoja naye.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Petro na wale waliokuwa pamoja naye walikuwa wamelemewa na usingizi; lakini walipokwisha amka waliuona utukufu wake, na wale wawili waliosimama pamoja naye.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Petro na wenzake walikuwa wanasinzia. Lakini waliamka na kuuona utukufu wa Yesu. Waliwaona pia watu wawili waliokuwa wamesimama pamoja naye.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Petro na wenzake walikuwa wamelemewa na usingizi mzito, hata hivyo waliamka, wakauona utukufu wake, wakawaona na wale watu wawili waliokuwa wamesimama pamoja naye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Petro na wenzake walikuwa wamelemewa na usingizi mzito, hata hivyo waliamka, wakauona utukufu wake, wakawaona na wale watu wawili waliokuwa wamesimama pamoja naye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Petro na wenzake waliokuwa wamelala usingizi mzito walipoamka, wakaona utukufu wa Yesu na wale watu wawili waliokuwa wamesimama pamoja naye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Petro na wenzake walikuwa wamelala usingizi mzito. Walipoamka, wakaona utukufu wa Isa na wale watu wawili waliokuwa wamesimama pamoja naye.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Petro na wale waliokuwa pamoja naye walikuwa wamelemewa na usingizi; lakini walipokwisha amka waliuona utukufu wake, na wale wawili waliosimama pamoja naye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Petro na wenzake walikuwa wamelemewa na usingizi mzito, hata hivyo waliamka, wakauona utukufu wake, wakawaona na wale watu wawili waliokuwa wamesimama pamoja naye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Petero na wenziwe walikuwa wamelemewa na usingizi. Walipoamka wakauona utukufu wake na wale waume wawili waliosimama naye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Petro na wale waliokuwa pamoja naye walikuwa wamelemewa na usingizi; lakini walipokwisha amka waliuona utukufu wake, na wale wawili waliosimama pamoja naye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa wakati ule Petro na wenzake walikuwa wamewezwa sana na usingizi; lakini wakaamuka, wakaona ule utukufu wa Yesu na wale watu wawili waliokuwa wakisimama pamoja naye.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Petro, nao waliokuwa pamoja nae, walikuwa wamelemewa sana na usingizi: lakini walipokwisha kuamka wakauona utukufu wake, na wale watu wawili, waliosimama pamoja nae.