Luke 9:34 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Petro alipokuwa akisema hayo, mara wingu likatokea na kuwafunika; na wingu hilo lilipowajia, wale wanafunzi waliogopa sana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipokuwa bado anazungumza, pakatokea wingu, likawafunika, nao wakaogopa walipoingia mle kwenye wingu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Alipokuwa akisema hayo, lilitokea wingu likawatia uvuli, wakaogopa walipoingia katika wingu hilo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Petro alipokuwa akisema mambo haya, wingu likaja, likawafunika wote. Petro, Yohana na Yakobo waliogopa walipofunikwa na wingu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Petro alipokuwa akisema hayo, mara wingu likatokea na kuwafunika; na wingu hilo lilipowajia, wale wanafunzi waliogopa sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Petro alipokuwa akisema hayo, mara wingu likatokea na kuwafunika; na wingu hilo lilipowajia, wale wanafunzi waliogopa sana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipokuwa bado anazungumza, pakatokea wingu likawafunika, nao wakaogopa walipoingia mle kwenye wingu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipokuwa bado anazungumza, pakatokea wingu, likawafunika, nao wakaogopa walipoingia mle kwenye wingu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Alipokuwa akisema hayo, lilitokea wingu likawatia uvuli, wakaogopa walipoingia katika wingu hilo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Petro alipokuwa akisema hayo, mara wingu likatokea na kuwafunika; na wingu hilo lilipowajia, wale wanafunzi waliogopa sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Angali akiyasema haya, pakawa na wingu, likawatia kivuli, wakashikwa na woga walipoingiwa na wingu lile.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Alipokuwa akisema hayo, lilitokea wingu likawatia uvuli, wakaogopa walipoingia katika wingu hilo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alipokuwa hajamaliza kusema, wingu likatokea na kuwafunika. Nao wanafunzi wale wakaogopa kwa kuona wamefunikwa na lile wingu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta alipokuwa akisema haya likawako wingu, likawatia uvuli; wakaogopa walipoingia katika lile wingu.