Luke 9:36 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya hiyo sauti kusikika, Yesu alionekana akiwa peke yake. Wanafunzi walikaa kimya juu ya tukio hilo, na wakati ule hawakumwambia mtu yeyote mambo hayo waliyoyaona.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya sauti hiyo kusema, walimkuta Isa akiwa peke yake. Wale wanafunzi wakalihifadhi jambo hili, wala kwa wakati huo hawakumwambia mtu yeyote yale waliyokuwa wameyaona.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na sauti hiyo ilipokwisha, Yesu alionekana yu peke yake. Nao wakanyamaza, wasitangaze kwa mtu siku zile lo lote katika hayo waliyoyaona.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sauti hiyo ilipomalizika, Yesu peke yake ndiye alikuwa pale. Petro, Yohana na Yakobo hawakusema chochote. Na kwa muda mrefu baada ya hilo, hawakumwambia mtu yeyote yale waliyoyaona.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baada ya hiyo sauti kusikika, Yesu alionekana akiwa peke yake. Wanafunzi walikaa kimya juu ya tukio hilo, na wakati ule hawakumwambia mtu yeyote mambo hayo waliyoyaona.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya hiyo sauti kusikika, Yesu alionekana akiwa peke yake. Wanafunzi walikaa kimya juu ya tukio hilo, na wakati ule hawakumwambia mtu yeyote mambo hayo waliyoyaona.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya sauti hiyo kusema, walimkuta Yesu akiwa peke yake. Wale wanafunzi wakalihifadhi jambo hili, wala kwa wakati huo hawakumwambia mtu ye yote yale waliyokuwa wameyaona.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya sauti hiyo kusema, walimkuta Isa akiwa peke yake. Wale wanafunzi wakalihifadhi jambo hili, wala kwa wakati huo hawakumwambia mtu yeyote yale waliyokuwa wameyaona.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na sauti hiyo ilipokwisha, Yesu alionekana yu peke yake. Nao wakanyamaza, wasitangaze kwa mtu siku zile lolote katika hayo waliyoyaona.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya hiyo sauti kusikika, Yesu alionekana akiwa peke yake. Wanafunzi walikaa kimya juu ya tukio hilo, na wakati ule hawakumwambia mtu yeyote mambo hayo waliyoyaona.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sauti hiyo iliposikilika, Yesu akaonekana, yuko peke yake. Siku zile wakanyamaza, wasimsimulie mtu hata moja lao hayo waliyoyaona.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na sauti hiyo ilipokwisha, Yesu alionekana yu peke yake. Nao wakanyamaza, wasitangaze kwa mtu siku zile lo lote katika hayo waliyoyaona.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma ya kusikilika kwa sauti ile, Yesu akaonekana amebaki peke yake. Wale wanafunzi wakachunga mambo hayo yote kwa siri wala hawakumwambia mutu neno katika siku zile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na sauti hii ilipokuja Yesu akaonekana peke yake. Nao wakanyamaza wasimwambie mtu siku zile neno lo lote la hayo waliyoyaona.