Luke 9:39 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Pepo huwa anamshambulia, na mara humfanya apige kelele; humtia kifafa, na povu likamtoka kinywani. Huendelea kumtesa sana, asimwache upesi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mara kwa mara pepo mchafu humpagaa na kumfanya apige mayowe, kisha humwangusha na kumtia kifafa hata akatokwa na povu kinywani. Huyo pepo mchafu anamtesa sana, na hamwachi ila mara chache.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tazama, pepo humpagaa, naye mara hupiga kelele; tena humtia kifafa, huku anatokwa na povu, wala hamwachi ila kwa shida, akimchubua-chubua.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Pepo mchafu humvaa na hupiga kelele, humtia kifafa na kumtoa povu mdomoni. Huendelea kumwumiza na hamwachi kirahisi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Pepo huwa anamshambulia, na mara humfanya apige kelele; humtia kifafa, na povu likamtoka kinywani. Huendelea kumtesa sana, asimwache upesi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Pepo huwa anamshambulia, na mara humfanya apige kelele; humtia kifafa, na povu likamtoka kinywani. Huendelea kumtesa sana, asimwache upesi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mara kwa mara pepo mchafu humpagaa na kumfanya apige kelele, kisha humwangusha na kumtia kifafa akatokwa na povu kinywani. Huyo pepo mchafu anamtesa sana na hamwachi ila mara chache.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mara kwa mara pepo mchafu humpagaa na kumfanya apige kelele, kisha humwangusha na kumtia kifafa hata akatokwa na povu kinywani. Huyo pepo mchafu anamtesa sana, na hamwachi ila mara chache.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tazama, pepo humpagaa, naye mara hupiga kelele; tena humtia kifafa, huku anatokwa na povu, wala hamwachi ila kwa shida, akimchubua-chubua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Pepo huwa anamshambulia, na mara humfanya apige kelele; humtia kifafa, na povu likamtoka kinywani. Huendelea kumtesa sana, asimwache upesi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tazama, pepo humpagaa, naye mara moja hulia kwa kukumbwa, mpaka akitoka pofu; akiisha kumlegeza hukawia kumwondokea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tazama, pepo humpagaa, naye mara hupiga kelele; tena humtia kifafa, huku anatokwa na povu, wala hamwachi ila kwa shida, akimchubua-chubua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Pepo anapomukamata, mara moja mutoto analalamika, na yule pepo anamutikisatikisa kwa nguvu hata pofu inamutoka. Huyo pepo hatoki ndani yake upesi, naye anamutesa sana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
na tazama, pepo humshika, nae marra hulia; tena humrarua, akatoka povu, wala hamtoki illa kwa shidda, akimchubuachubua.