Luke 9:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wakikataa kuwakaribisha, tokeni katika mji huo, nanyi mnapotoka kunguteni mavumbi miguuni mwenu kama onyo kwao.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama watu wasipowakaribisha, mnapoondoka katika mji wao, kung’uteni mavumbi kutoka miguu yenu ili kuwa ushuhuda dhidi yao.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wale wasiowakaribisha, mtokapo katika mji huo, yakung'uteni hata mavumbi ya miguuni mwenu, kuwa ushuhuda juu yao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ikiwa watu katika mji mtakaoingia hawatawakaribisha, nendeni nje ya mji na kuyakung'uta mavumbi miguuni mwenu kama onyo kwao.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Watu wakikataa kuwakaribisha, tokeni katika mji huo, nanyi mnapotoka kung'uteni mavumbi miguuni mwenu kama onyo kwao.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wakikataa kuwakaribisha, tokeni katika mji huo, nanyi mnapotoka kung'uteni mavumbi miguuni mwenu kama onyo kwao.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama watu wasipowakaribisha, mnapoondoka katika mji wao, kung'uteni mavumbi miguuni mwenu kuwa ushuhuda dhidi yao.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama watu wasipowakaribisha, mnapoondoka katika mji wao, kung’uteni mavumbi kutoka kwenye miguu yenu ili kuwa ushuhuda dhidi yao.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wale wasiowakaribisha, mtokapo katika mji huo, yakung'uteni hata mavumbi ya miguuni mwenu, kuwa ushuhuda juu yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wakikataa kuwakaribisha, tokeni katika mji huo, nanyi mnapotoka kunguteni mavumbi miguuni mwenu kama onyo kwao.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wote wasiowapokea, basi, utokeni mji wao na kuyakung'uta mavumbi yaliyoishika miguu yenu, yaje yanishuhudie kwao!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wale wasiowakaribisha, mtokapo katika mji huo, yakung’uteni hata mavumbi ya miguuni mwenu, kuwa ushuhuda juu yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na katika muji wowote watu watakapokataa kuwakaribisha, mutoke kule na mukungute mavumbi toka juu ya miguu yenu. Jambo hili litakuwa ushuhuda juu yao.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na wo wote wasiowakarihisheni, mtokapo katika mji ule, yakungʼuteni mavumbi ya miguuni mwenu illi kuwa ushuhuda juu yao.