Malachi 1:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema, “Laiti angepatikana mtu mmoja miongoni mwenu ambaye angefunga milango ya hekalu ili msiwashe moto usiokubalika kwenye madhabahu yangu! Sipendezwi nanyi na sitaikubali tambiko yoyote mnayonitolea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Laiti mmoja wenu angeifunga milango ya Hekalu, ili msije mkawasha moto usiokuwa na faida juu ya madhabahu yangu! Sina furaha nanyi,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, “nami sitaikubali sadaka toka mikononi mwenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Laiti angekuwapo kwenu mtu mmoja wa kuifunga milango; msije mkawasha moto bure madhabahuni pangu! Sina furaha kwenu, asema Bwana wa majeshi, wala sitakubali dhabihu yo yote mikononi mwenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema, “Laiti angepatikana mtu mmoja miongoni mwenu ambaye angefunga milango ya hekalu ili msiwashe moto usiokubalika kwenye madhabahu yangu! Sipendezwi nanyi na sitaikubali tambiko yoyote mnayonitolea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Laiti mmoja wenu angalifunga milango ya Hekalu, ili msije mkawasha moto usiokuwa na faida juu ya madhabahu yangu! Sina furaha nanyi,” asema BWANA Mwenye Nguvu Zote, “nami sitaikubali sadaka toka mikononi mwenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Laiti mmoja wenu angalifunga milango ya Hekalu, ili msije mkawasha moto usiokuwa na faida juu ya madhabahu yangu! Sina furaha nanyi,” asema bwana Mwenye Nguvu Zote, “nami sitaikubali sadaka toka mikononi mwenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Laiti angekuwapo kwenu mtu mmoja wa kuifunga milango; msije mkawasha moto bure madhabahuni pangu! Sina furaha kwenu, asema BWANA wa majeshi, wala sitakubali dhabihu yoyote mikononi mwenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema, “Laiti angepatikana mtu mmoja miongoni mwenu ambaye angefunga milango ya hekalu ili msiwashe moto usiokubalika kwenye madhabahu yangu! Sipendezwi nanyi na sitaikubali tambiko yoyote mnayonitolea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vingekuwa vyema, kama mtu wa kwenu angeifunga milango, msije kuwasha moto bure mezani pangu pa kutambikia! Sipendezwi kabisa nanyi, wala sipendezwi na vipaji vya tambiko vitokavyo mikononi mwenu; ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Laiti angekuwapo kwenu mtu mmoja wa kuifunga milango; msije mkawasha moto bure madhabahuni pangu! Sina furaha kwenu, asema BWANA wa majeshi, wala sitakubali dhabihu yo yote mikononi mwenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Heri kungepatikana mutu mumoja kati yenu ambaye angefunga milango ya hekalu kusudi musiwashe moto usiokubaliwa kwenye mazabahu yangu! Sipendezwi nanyi na sitaikubali sadaka yoyote munayonitolea.