Malachi 1:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnasema, ‘Mambo haya yametuchosha mno,’ na mnanidharau. Mnaniletea tambiko za wanyama mliowapata kwa unyang'anyi, au walio vilema au wagonjwa. Je, nipokee tambiko hizo mikononi mwenu? Mimi Mwenyezi-Mungu nauliza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nanyi mnasema, ‘Mzigo gani huu!’ Nanyi mnaidharau kwa kiburi,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. “Mnapowaleta wanyama mliopokonya kwa nguvu, walio vilema au walio wagonjwa na kuwatoa kama dhabihu, je, niwakubali kutoka mikononi mwenu?” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena mwasema, Tazama, jambo hili linatuchokesha namna gani! Nanyi mmelidharau, asema Bwana wa majeshi; nanyi mmeleta kitu kilichopatikana kwa udhalimu, na kilema, na kilicho kigonjwa; ndivyo mnavyoleta sadaka; je! Niikubali hii mikononi mwenu? Asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnasema, ‘Mambo haya yametuchosha mno,’ na mnanidharau. Mnaniletea tambiko za wanyama mliowapata kwa unyang'anyi, au walio vilema au wagonjwa. Je, nipokee tambiko hizo mikononi mwenu? Mimi Mwenyezi-Mungu nauliza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nanyi mnasema, ‘Mzigo gani huu!’ Nanyi mnaidharau kwa kiburi,” asema BWANA Mwenye Nguvu Zote. “Wakati mnapowaleta wanyama mliopokonya kwa nguvu, vilema au walio wagonjwa na kuwatoa kama dhabihu, je, niwakubali kutoka mikononi mwenu?” asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nanyi mnasema, ‘Mzigo gani huu!’ Nanyi mnaidharau kwa kiburi,” asema bwana Mwenye Nguvu Zote. “Wakati mnapowaleta wanyama mliopokonya kwa nguvu, walio vilema au walio wagonjwa na kuwatoa kama dhabihu, je, niwakubali kutoka mikononi mwenu?” asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena mwasema, Tazama, jambo hili linatuchokesha namna gani! Nanyi mmelidharau, asema BWANA wa majeshi; nanyi mmeleta kitu kilichopatikana kwa udhalimu, na kilema, na kilicho kigonjwa; ndivyo mnavyoleta sadaka; je! Niikubali hii mikononi mwenu? Asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnasema, ‘Mambo haya yametuchosha mno,’ na mnanidharau. Mnaniletea tambiko za wanyama mliowapata kwa unyang'anyi, au walio vilema au wagonjwa. Je, nipokee tambiko hizo mikononi mwenu? Mimi Mwenyezi-Mungu nauliza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena anasema Bwana Mwenye vikosi: Mwasema: Tazameni, tunavyosumbuka! kisha mwazinung'unikia kazi zenu na kuleta nyama aliyenyang'anywa au achechemeaye au auguaye, mmtoe kuwa ng'ombe ya tambiko; basi, nipendezwe na vipaji hivyo vitokavyo mikononi mwenu? ndivyo, Bwana anavyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena mwasema, Tazama, jambo hili linatuchokesha namna gani! Nanyi mmelidharau, asema BWANA wa majeshi; nanyi mmeleta kitu kilichopatikana kwa udhalimu, na kilema, na kilicho kigonjwa; ndivyo mnavyoleta sadaka; je! Niikubali hii mikononi mwenu? Asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Munasema: Mambo haya yametuchokesha sana na munanizarau. Munaniletea sadaka za nyama muliopata kwa njia ya kunyanganya, au wanaokua vilema au wagonjwa. Basi, nipokee sadaka hizo toka katika mikono yenu?