Malachi 1:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnaponitolea tambiko ya mnyama kipofu, au kilema, au mgonjwa, je, huo si uovu? Je, mtawala atapendezwa au kukufanyia hisani ukimpa zawadi ya mnyama kama huyo?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mnapoleta dhabihu za wanyama walio vipofu, je, hilo si kosa? Mnapoleta dhabihu zilizo vilema au wanyama wagonjwa, je, hilo si kosa? Jaribuni kuvitoa kwa mtawala wenu! Je, angefurahishwa nanyi? Je, atawakubalia?” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena mtoapo sadaka aliye kipofu, si vibaya? Na mtoapo sadaka walio vilema na wagonjwa, si vibaya? Haya! Mtolee liwali wako; je! Atakuwa radhi nawe? Au atakukubali nafsi yako? Asema Bwana wa majeshi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnaponitolea tambiko ya mnyama kipofu, au kilema, au mgonjwa, je, huo si uovu? Je, mtawala atapendezwa au kukufanyia hisani ukimpa zawadi ya mnyama kama huyo?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati mletapo dhabihu wanyama walio vipofu, je, hilo si kosa? Mnapoleta dhabihu zilizo vilema au wanyama wagonjwa, je, hilo si kosa? Jaribuni kuvitoa kwa mtawala wenu! Je, angefurahiwa nanyi? Je, atawakubalia?” Asema BWANA Mwenye Nguvu Zote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati mletapo dhabihu za wanyama walio vipofu, je, hilo si kosa? Mnapoleta dhabihu zilizo vilema au wanyama wagonjwa, je, hilo si kosa? Jaribuni kuvitoa kwa mtawala wenu! Je, angefurahishwa nanyi? Je, atawakubalia?” asema bwana Mwenye Nguvu Zote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena mtoapo sadaka aliye kipofu, si vibaya? Na mtoapo sadaka walio vilema na wagonjwa, si vibaya? Haya! Mtolee mtawala wako; Je, Atakuwa radhi nawe? Au atakukubali nafsi yako? Asema BWANA wa majeshi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnaponitolea tambiko ya mnyama kipofu, au kilema, au mgonjwa, je, huo si uovu? Je, mtawala atapendezwa au kukufanyia hisani ukimpa zawadi ya mnyama kama huyo?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena mkileta nyma kipofu kuwa ng'ombe ya tambiko, si vibaya? Au mkileta achechemeaye au aliyeugua, si vibaya? Haya! Umpelekee mtawala nchi vyako vilivyo hivyo, uone, kama atapendezwa na wewe, akupendelee! ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena mtoapo sadaka aliye kipofu, si vibaya? Na mtoapo sadaka walio vilema na wagonjwa, si vibaya? Haya! Mtolee liwali wako; je! Atakuwa radhi nawe? Au atakukubali nafsi yako? Asema BWANA wa majeshi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Munaponitolea sadaka ya nyama anayekuwa kipofu, au kilema, au mugonjwa, huo si uovu? Mutawala atapendezwa au kukutendea mema ukimupa zawadi ya nyama kama yule? –Ni Yawe wa majeshi anayesema hivyo.