Malachi 2:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Zaidi ya hayo yote, mnaifunika madhabahu ya Mwenyezi-Mungu kwa machozi yenu, mkilia na kuomboleza kwa sababu yeye hazikubali tena tambiko mnazomtolea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kitu kingine mnachokifanya: Mnaifurikisha madhabahu ya Mwenyezi Mungu kwa machozi. Mnalia na kuugua kwa sababu yeye haziangalii tena sadaka zenu wala hazikubali kwa furaha kutoka mikononi mwenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena mnatenda haya nayo; mnaifunikiza madhabahu ya Bwana kwa machozi, kwa kulia na kwa kuugua, hata asiiangalie tena hiyo dhabihu, wala kuitakabali mikononi mwenu na kuiridhia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Zaidi ya hayo yote, mnaifunika madhabahu ya Mwenyezi-Mungu kwa machozi yenu, mkilia na kuomboleza kwa sababu yeye hazikubali tena tambiko mnazomtolea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kitu kingine mnachokifanya: Mnaifurikisha madhabahu ya BWANA kwa machozi. Mnalia na kuugua kwa sababu yeye haziangalii tena sadaka zenu wala hazikubali kwa furaha kutoka mikononi mwenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kitu kingine mnachokifanya: Mnaifurikisha madhabahu ya bwana kwa machozi. Mnalia na kuugua kwa sababu yeye haziangalii tena sadaka zenu wala hazikubali kwa furaha kutoka mikononi mwenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena mnatenda haya nayo; mnaifunikiza madhabahu ya BWANA kwa machozi, kwa kulia na kwa kuugua, hata asiiangalie tena hiyo dhabihu, wala kuitakabali mikononi mwenu na kuiridhia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Zaidi ya hayo yote, mnaifunika madhabahu ya Mwenyezi-Mungu kwa machozi yenu, mkilia na kuomboleza kwa sababu yeye hazikubali tena tambiko mnazomtolea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena hili ni la pili mnalolifanya: meza ya kumtambikia Bwana mnaifunika kwa machozi yao wamliliao na kupiga kite, asitazame tena kipaji cho chote cha tambiko, wala asipokee mikononi mwenu cho chote cha kumpendeza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena mnatenda haya nayo; mnaifunikiza madhabahu ya BWANA kwa machozi, kwa kulia na kwa kuugua, hata asiiangalie tena hiyo dhabihu, wala kuitakabali mikononi mwenu na kuiridhia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Zaidi ya hayo yote, munaifunika mazabahu ya Yawe kwa machozi yenu, mukilia na kuomboleza kwa sababu yeye hazikubali tena sadaka munazomutolea.