Malachi 2:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mmemchosha Mwenyezi-Mungu kwa maneno yenu matupu. Hata hivyo, mnasema, “Tumemchoshaje?” Mmemchosha mnaposema, “Mwenyezi-Mungu huwaona kuwa wema watu wanaotenda maovu; tena anawapenda.” Au mnapouliza, “Yuko wapi yule Mungu mwenye haki?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mmemchosha Mwenyezi Mungu kwa maneno yenu. Nanyi mnauliza, “Tumemchosha kwa namna gani?” Mmemchosha kwa kusema, “Wote watendao mabaya ni wema machoni pa Mwenyezi Mungu, naye anapendezwa nao” au “Mungu wa haki yuko wapi?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mmemchokesha Bwana kwa maneno yenu. Lakini ninyi mwasema, Tumemchokesha kwa maneno gani? Kwa kuwa mwasema, Kila atendaye mabaya ni mwema machoni pa Bwana, naye huwafurahia watu hao, au, Mungu mwenye kuhukumu yuko wapi?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mmemchosha Mwenyezi-Mungu kwa maneno yenu matupu. Hata hivyo, mnasema, “Tumemchoshaje?” Mmemchosha mnaposema, “Mwenyezi-Mungu huwaona kuwa wema watu wanaotenda maovu; tena anawapenda.” Au mnapouliza, “Yuko wapi yule Mungu mwenye haki?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mmemchosha BWANA kwa maneno yenu. Nanyi mnauliza, “Tumemchosha kwa namna gani?” Mmemchosha kwa kusema, “Wote watendao mabaya ni wema machoni pa BWANA, naye anapendezwa nao” au “Mungu wa haki yuko wapi?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mmemchosha bwana kwa maneno yenu. Nanyi mnauliza, “Tumemchosha kwa namna gani?” Mmemchosha kwa kusema, “Wote watendao mabaya ni wema machoni pa bwana, naye anapendezwa nao” au “Mungu wa haki yuko wapi?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mmemchokesha BWANA kwa maneno yenu. Lakini ninyi mwasema, Tumemchokesha kwa maneno gani? Kwa kuwa mwasema, Kila atendaye mabaya ni mwema machoni pa BWANA, naye huwafurahia watu hao, au, Mungu mwenye haki yuko wapi?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mmemchosha Mwenyezi-Mungu kwa maneno yenu matupu. Hata hivyo, mnasema, “Tumemchoshaje?” Mmemchosha mnaposema, “Mwenyezi-Mungu huwaona kuwa wema watu wanaotenda maovu; tena anawapenda.” Au mnapouliza, “Yuko wapi yule Mungu mwenye haki?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mmemchokesha Bwana kwa maneno yenu, mkiuliza: Tumemchokesha kwa nini? Ni kwa kusema kwenu; kila afanyaye mabaya ni mwema machoni pa Bwana, nao walio hivyo ndio, anaopendezwa nao! Au mkiuliza: Yuko wapi Mungu anayepatiliza?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mmemchokesha BWANA kwa maneno yenu. Lakini ninyi mwasema, Tumemchokesha kwa maneno gani? Kwa kuwa mwasema, Kila atendaye mabaya ni mwema machoni pa BWANA, naye huwafurahia watu hao, au, Mungu mwenye kuhukumu yuko wapi?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mumemuchokesha Yawe kwa maneno yenu matupu. Hata hivyo, munasema: Tumemuchokesha namna gani? Mumemuchokesha munaposema: Yawe anawaona kuwa wazuri watu wanaotenda mabaya; tena anawapenda. Au munapouliza: Yuko wapi yule Mungu mwenye haki?