Malachi 2:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Bali nyinyi makuhani mmegeuka mkaiacha njia ya haki. Mafundisho yenu yamewaongoza watu wengi katika kutenda mabaya. Mmelivunja agano nililofanya nanyi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mmegeuka mkaiacha njia, na kwa mafundisho yenu mmesababisha wengi kujikwaa. Mmevunja agano na Lawi,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bali ninyi mmegeuka mkaiacha njia; mmewakwaza watu wengi katika sheria; mmeliharibu agano la Lawi, asema Bwana wa majeshi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Bali nyinyi makuhani mmegeuka mkaiacha njia ya haki. Mafundisho yenu yamewaongoza watu wengi katika kutenda mabaya. Mmelivunja agano nililofanya nanyi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mmegeuka mkaiacha njia na kwa mafundisho yenu mmesababisha wengi kujikwaa, mmevunja agano na Lawi,” asema BWANA Mwenye Nguvu Zote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mmegeuka mkaiacha njia, na kwa mafundisho yenu mmesababisha wengi kujikwaa. Mmevunja agano na Lawi,” asema bwana Mwenye Nguvu Zote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bali ninyi mmegeuka mkaiacha njia; mmewakwaza watu wengi katika sheria; mmeliharibu agano la Lawi, asema BWANA wa majeshi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Bali nyinyi makuhani mmegeuka mkaiacha njia ya haki. Mafundisho yenu yamewaongoza watu wengi katika kutenda mabaya. Mmelivunja agano nililofanya nanyi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini ninyi mmeiacha njia hiyo, mkakwaza wengi, wasiyashike Maonyo, mkalivunja agano, nililolifanya na Lawi; ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bali ninyi mmegeuka mkaiacha njia; mmewakwaza watu wengi katika sheria; mmeliharibu agano la Lawi, asema BWANA wa majeshi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ninyi makuhani mumegeuka na kuacha njia ya haki. Mafundisho yenu yamewaongoza watu wengi katika kutenda mabaya. Mumelivunja agano nililofanya nanyi.