Malachi 3:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Leteni ghalani mwangu zaka yote, ili nyumbani mwangu kuwe na chakula cha kutosha. Kisha mwaweza kunijaribu. Nijaribuni namna hiyo nanyi mtaona kama sitayafungua madirisha ya mbinguni na kuwatiririshia baraka tele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Leteni zaka kamili ghalani, ili kuwe na chakula katika nyumba yangu. Nijaribuni katika hili,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, “nanyi mwone kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni baraka nyingi hata mkose nafasi ya kutosha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Leteni ghalani mwangu zaka yote, ili nyumbani mwangu kuwe na chakula cha kutosha. Kisha mwaweza kunijaribu. Nijaribuni namna hiyo nanyi mtaona kama sitayafungua madirisha ya mbinguni na kuwatiririshia baraka tele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu. Nijaribuni katika hili,” asema BWANA Mwenye Nguvu Zote, “nanyi mwone kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni baraka nyingi mpaka mkose nafasi ya kutosha au la.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Leteni zaka kamili ghalani, ili kuwe na chakula katika nyumba yangu. Nijaribuni katika hili,” asema bwana Mwenye Nguvu Zote, “nanyi mwone kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni baraka nyingi mpaka mkose nafasi ya kutosha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Leteni ghalani mwangu zaka yote, ili nyumbani mwangu kuwe na chakula cha kutosha. Kisha mwaweza kunijaribu. Nijaribuni namna hiyo nanyi mtaona kama sitayafungua madirisha ya mbinguni na kuwatiririshia baraka tele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yapelekeni mafungu yote ya kumi mle nyumbani, kilimbiko kilimo, yawe vilaji vya Nyumbani mwangu! Kanijaribuni hivyo, kama sitawafunulia madirisha ya mbinguni, nikiwamwagia mbaraka isiyopimika kwa kufurika; ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mulete katika gala yangu zaka yote, kusudi katika nyumba yangu kuwe chakula cha kutosha. Kisha munaweza kunijaribu. Munipime namna hiyo nanyi mutaona kama sitayafungua madirisha ya mbinguni na kuwatiririshia baraka tele.