Malachi 3:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo watu wanaomcha Mwenyezi-Mungu walipozungumza wao kwa wao, naye Mwenyezi-Mungu akasikia mazungumzo yao. Mbele yake kikawekwa kitabu ambamo iliandikwa kumbukumbu ya wale wanaomcha na kumheshimu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo wale waliomcha Mwenyezi Mungu wakasemezana wao kwa wao, naye Mwenyezi Mungu akasikiliza na akasikia. Kitabu cha kumbukumbu kikaandikwa mbele yake kuhusu wale ambao walimcha Mwenyezi Mungu na kuliheshimu jina lake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo wale waliomcha Bwana waliposemezana wao kwa wao. Naye Bwana akasikiliza, akasikia; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao waliomcha Bwana, na kulitafakari jina lake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo watu wanaomcha Mwenyezi-Mungu walipozungumza wao kwa wao, naye Mwenyezi-Mungu akasikia mazungumzo yao. Mbele yake kikawekwa kitabu ambamo iliandikwa kumbukumbu ya wale wanaomcha na kumheshimu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo wale waliomcha BWANA wakasemezana wao kwa wao, naye BWANA akasikiliza naye akasikia. Kitabu cha kumbukumbu kikaandikwa mbele yake kuhusu wale ambao walimcha BWANA na kuliheshimu jina lake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo wale waliomcha bwana wakasemezana wao kwa wao, naye bwana akasikiliza na akasikia. Kitabu cha kumbukumbu kikaandikwa mbele yake kuhusu wale ambao walimcha bwana na kuliheshimu jina lake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo wale waliomcha BWANA waliposemezana wao kwa wao. Naye BWANA akasikiliza, akasikia; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao waliomcha BWANA, na kulitafakari jina lake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo watu wanaomcha Mwenyezi-Mungu walipozungumza wao kwa wao, naye Mwenyezi-Mungu akasikia mazungumzo yao. Mbele yake kikawekwa kitabu ambamo iliandikwa kumbukumbu ya wale wanaomcha na kumheshimu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo, wamchao Bwana walipoongeana kila mtu na mwenziwe, Bwana alitega sikio, akasikiliza; mbele yake kikaandikwa kitabu cha ukumbusho wao waliomcha Bwana na kulikumbuka Jina lake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo wale waliomcha BWANA waliposemezana wao kwa wao. Naye BWANA akasikiliza, akasikia; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao waliomcha BWANA, na kulitafakari jina lake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu watu wanaomutii Yawe walizungumuza wao kwa wao, naye Yawe akasikia mazungumuzo yao. Mbele yake kukawekwa kitabu ambamo uliandikwa ukumbusho wa wale wanaomutii na kumuheshimu.