Malachi 3:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tangu wakati wa wazee wenu, mmezidharau kanuni zangu wala hamkuzifuata. Basi, mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu Mkuu nasema: Nirudieni, nami nitawageukieni. Lakini nyinyi mnauliza, ‘Tutakurudia namna gani?’ Nami nawaulizeni,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tangu wakati wa baba zenu mmegeukia mbali na amri zangu nanyi hamkuzishika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. “Lakini mnauliza, ‘Tutarudi kwa namna gani?’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi, asema Bwana wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tangu wakati wa wazee wenu, mmezidharau kanuni zangu wala hamkuzifuata. Basi, mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu Mkuu nasema: nirudieni, nami nitawageukieni. Lakini nyinyi mnauliza, ‘Tutakurudia namna gani?’ Nami nawaulizeni,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tangu wakati wa baba zenu mmegeukia mbali na amri zangu nanyi hamkuzishika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi,” asema BWANA Mwenye Nguvu Zote. “Lakini mnauliza, ‘Tutarudi kwa namna gani?’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tangu wakati wa baba zenu mmegeukia mbali na amri zangu nanyi hamkuzishika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi,” asema bwana Mwenye Nguvu Zote. “Lakini mnauliza, ‘Tutarudi kwa namna gani?’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi, asema BWANA wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tangu wakati wa wazee wenu, mmezidharau kanuni zangu wala hamkuzifuata. Basi, mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu Mkuu nasema: Nirudieni, nami nitawageukieni. Lakini nyinyi mnauliza, ‘Tutakurudia namna gani?’ Nami nawaulizeni,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tangu siku za baba zenu mmeyaacha maongozi yangu, hamkuyashika, myaangalie. Rudini kwangu! Ndipo, nami nitakaporudi kwenu; ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema. Nanyi mnauliza: Turudi kwa njia gani?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi, asema BWANA wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tangu wakati wa babu zenu, mumeyazarau masharti yangu wala hamukuyafuata. Munirudilie, nami nitawageukia. Lakini ninyi munaniuliza: Tutakurudilia namna gani?