Malachi 4:1 — Compare Translations

10 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema: “Tazama, siku yaja, nayo inawaka kama tanuri. Wenye kiburi na waovu wote watatupwa humo na kuteketea kama mabua makavu; watateketea kabisa pasibaki hata alama.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hakika siku inakuja, itawaka kama tanuru. Wote wenye kiburi na watenda maovu watakuwa mabua makavu, na siku ile inayokuja itawawasha moto,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. “Hakuna mzizi wala tawi litakalosalia kwao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema Bwana wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema: “Tazama, siku yaja, nayo inawaka kama tanuri. Wenye kiburi na waovu wote watatupwa humo na kuteketea kama mabua makavu; watateketea kabisa pasibaki hata alama.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hakika siku inakuja, itawaka kama tanuru. Wote wenye kiburi na kila mtenda mabaya watakuwa mabua makavu na siku ile inayokuja itawawasha moto,” asema BWANA Mwenye Nguvu Zote. “Hakuna mzizi wala tawi litakalosalia kwao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hakika siku inakuja, itawaka kama tanuru. Wote wenye kiburi na kila mtenda mabaya watakuwa mabua makavu, na siku ile inayokuja itawawasha moto,” asema bwana Mwenye Nguvu Zote. “Hakuna mzizi wala tawi litakalosalia kwao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuri; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema BWANA wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema: “Tazama, siku yaja, nayo inawaka kama tanuri. Wenye kiburi na waovu wote watatupwa humo na kuteketea kama mabua makavu; watateketea kabisa pasibaki hata alama.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Kwani mtaiona hiyo siku, ikija na kuwaka moto kama wa tanuru; ndipo, waliomsahau Mungu nao wote waliofanya maovu watakapokuwa makapi, siku hiyo ijayo itakapoyateketeza, isisaze wala mizizi wala matawi yao hao; ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema BWANA wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.