Mark 1:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alipokuwa anapita kando ya ziwa Galilaya, aliwaona wavuvi wawili: Simoni na Andrea ndugu yake wakivua samaki kwa wavu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa alipokuwa akitembea kando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona Simoni na Andrea nduguye wakizitupa nyavu zao baharini, kwa kuwa walikuwa wavuvi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye alipokuwa akipita kando ya bahari ya Galilaya, akamwona Simoni na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alipokuwa akitembea kando kando ya Ziwa Galilaya, Yesu alimwona Simoni na Andrea ndugu yake. Hao walikuwa wavuvi na walikuwa wakizitupa nyavu zao ziwani kukamata samaki.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Alipokuwa anapita kando ya ziwa Galilaya, aliwaona wavuvi wawili: Simoni na Andrea ndugu yake wakivua samaki kwa wavu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alipokuwa anapita kando ya ziwa Galilaya, aliwaona wavuvi wawili: Simoni na Andrea ndugu yake wakivua samaki kwa wavu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu alipokuwa akitembea kandokando ya Bahari ya Galilaya alimwona Simoni na Andrea nduguye wakizitupa nyavu zao baharini, kwa kuwa hawa wawili walikuwa wavuvi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa alipokuwa akitembea kando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona Simoni na Andrea nduguye wakizitupa nyavu zao baharini, kwa kuwa wao walikuwa wavuvi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye alipokuwa akipita kando ya bahari ya Galilaya, akamwona Simoni na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alipokuwa anapita kando ya ziwa Galilaya, aliwaona wavuvi wawili: Simoni na Andrea ndugu yake wakivua samaki kwa wavu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye alipokuwa akitembea kandokando ya bahari ya Galilea, akamwona Simoni na Anderea, nduguye Simoni, wakitupa nyavu zao baharini, kwani walikuwa wavuvi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye alipokuwa akipita kando ya bahari ya Galilaya, akamwona Simoni na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati Yesu alipokuwa akitembea pembeni ya ziwa la Galilaya akawaona wavuvi wawili, waliokuwa wandugu za tumbo: Simoni na ndugu yake Andrea. Walikuwa wakitupa nyavu katika ziwa lile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nae akipita kando ya bahari ya Galilaya, akamwona Simon na Andrea ndugu yake, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi.