Mark 1:2 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ilianza kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Mungu alisema, ‘Namtuma mjumbe wangu akutangulie, ambaye atakutayarishia njia yako.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Tazama, nitamtuma mjumbe wangu mbele yako, atakayetengeneza njia mbele yako”:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kama ilivyoandikwa katika nabii Isaya, Tazama, namtuma mjumbe wangu Mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia yako.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
zilianza kama vile Nabii Isaya alivyosema zitaanza, aliandika, “Sikiliza! Nitamtuma mjumbe mbele yako. Yeye ataandaa njia kwa ajili yako.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ilianza kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Tazama, namtuma mjumbe wangu akutangulie; yeye atakutayarishia njia yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ilianza kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Mungu alisema, ‘Namtuma mjumbe wangu akutangulie, ambaye atakutayarishia njia yako.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele yako, yeye atakayeitengeneza njia yako”:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Tazama, nitamtuma mjumbe wangu mbele yako, atakayetengeneza njia mbele yako”:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kama ilivyoandikwa katika nabii Isaya, Tazama, namtuma mjumbe wangu Mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ilianza kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Mungu alisema, ‘Namtuma mjumbe wangu akutangulie, ambaye atakutayarishia njia yako.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kama ulivyoandikwa na mfumbuaji Yesaya: Utaniona mimi, nikimtuma mjumbe wangu, akutangulie, aitengeneze njia yako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kama ilivyoandikwa katika nabii Isaya, Tazama, namtuma mjumbe wangu Mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na imeandikwa hivi katika kitabu cha nabii Isaya: “Mungu anasema: ‘Ninamutuma mujumbe wangu akutangulie, kusudi akutengenezee njia.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kama ilivyoandikwa katika chuo cha manabii, Angalia, mimi namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, Atakaefanyiza njia yako mbele yako.