Mark 1:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sauti ya mtu anaita jangwani: ‘Mtayarishieni Bwana njia yake, nyosheni barabara zake.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Itengenezeni njia ya Mwenyezi Mungu, yanyoosheni mapito yake.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
“Kuna mtu anayeipaza sauti yake toka nyikani: ‘Tayarisheni njia kwa ajili ya Bwana; nyoosheni njia kwa ajili yake.’”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sauti ya mtu imesikika jangwani: Mtayarishieni Bwana njia yake, nyoosheni mapito yake.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sauti ya mtu anaita jangwani: ‘Mtayarishieni Bwana njia yake, nyosheni barabara zake.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“sauti ya mtu aliaye nyikani. ‘Itengenezeni njia ya Bwana, yanyosheni mapito yake.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“sauti ya mtu aliaye nyikani. ‘Itengenezeni njia ya Mwenyezi Mungu, yanyoosheni mapito yake.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sauti ya mtu anaita jangwani: ‘Mtayarishieni Bwana njia yake, nyosheni barabara zake.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Iko sauti ya mtu apigaye mbiu nyikani: Itengenezeni njia ya Bwana! Yanyosheni mapito yake!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sauti inatangaza katika jangwa: ‘Mutengeneze njia ya Bwana, munyooshe pahali atakapopita!’ ”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Sauti yake aliae jangwani, Itengenezeni njia ya Bwana, Nyosheni mapito yake.