Mark 1:30 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, mama mmoja, mkwewe Simoni, alikuwa kitandani ana homa kali. Wakamwarifu Yesu mara alipowasili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mama mkwe wa Simoni alikuwa kitandani, ana homa, nao wakamweleza Isa habari zake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye mkwewe Simoni, mamaye mkewe, alikuwa kitandani, hawezi homa; na mara wakamwambia habari zake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mara Yesu alipoingia ndani ya nyumba watu wakamweleza kuwa mama mkwe wake Simoni alikuwa mgonjwa sana na alikuwa amepumzika kitandani kwa sababu alikuwa na homa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, mama mmoja, mkwewe Simoni, alikuwa kitandani ana homa kali. Wakamwarifu Yesu mara alipowasili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, mama mmoja, mkwewe Simoni, alikuwa kitandani ana homa kali. Wakamwarifu Yesu mara alipowasili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mama mkwe wa Simoni alikuwa kitandani, ana homa, nao wakamweleza Yesu habari zake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mama mkwe wa Simoni alikuwa kitandani, ana homa, nao wakamweleza Isa habari zake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye mkwewe Simoni, mamaye mkewe, alikuwa kitandani, akiugua homa; na mara wakamwambia habari zake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, mama mmoja, mkwewe Simoni, alikuwa kitandani ana homa kali. Wakamwarifu Yesu mara alipowasili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye mama ya mkewe Simoni alikuwa amelala kwa kuwa na homa. Papo hapo, walipomwambia, alivyokuwa,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye mkwewe Simoni, mamaye mkewe, alikuwa kitandani, hawezi homa; na mara wakamwambia habari zake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mama mukwe wa Simoni alikuwa katika kitanda, kwa sababu alikuwa na homa. Wakati Yesu alipofika pale, mara moja wakamupasha habari ya ugonjwa wake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mama wa mkewe Simon alikuwa kitandani, hawezi homa;