Mark 1:34 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Yesu akawaponya watu wengi waliokuwa na magonjwa mbalimbali; aliwafukuza pepo wengi, lakini hakuwaruhusu kusema kitu maana walikuwa wanamjua yeye ni nani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akawaponya watu wengi waliokuwa na magonjwa ya aina mbalimbali. Akawatoa pepo wachafu wengi, lakini hakuwaacha hao pepo wachafu waseme, kwa sababu walimjua yeye ni nani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaponya wengi waliokuwa na maradhi mbalimbali, akatoa pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu walimjua.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Naye akawaponya watu waliokuwa na magonjwa ya kila aina, na kufukuza mashetani wengi. Lakini yeye hakuyaruhusu mashetani kusema, kwa sababu yalimjua.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naye Yesu akawaponya watu wengi waliokuwa na magonjwa mbalimbali; aliwafukuza pepo wengi, lakini hakuwaruhusu kusema kitu maana walikuwa wanamjua yeye ni nani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Yesu akawaponya watu wengi waliokuwa na magonjwa mbalimbali; aliwafukuza pepo wengi, lakini hakuwaruhusu kusema kitu maana walikuwa wanamjua yeye ni nani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akawaponya watu wengi waliokuwa na magonjwa ya aina mbalimbali. Akawatoa pepo wachafu wengi, lakini hakuwaacha hao pepo wachafu waseme kwa sababu walimjua kuwa yeye ni nani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akawaponya watu wengi waliokuwa na magonjwa ya aina mbalimbali. Akawatoa pepo wachafu wengi, lakini hakuwaacha hao pepo wachafu waseme, kwa sababu walimjua yeye ni nani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaponya wengi waliokuwa na maradhi mbalimbali, akatoa pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu walimjua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Yesu akawaponya watu wengi waliokuwa na magonjwa mbalimbali; aliwafukuza pepo wengi, lakini hakuwaruhusu kusema kitu maana walikuwa wanamjua yeye ni nani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawaponya wengi waliokuwa hawawezi, wenye magonjwa mengi, akafukuza pepo wengi akiwakataza pepo kusema, ya kuwa walimjua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaponya wengi waliokuwa na maradhi mbalimbali, akatoa pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu walimjua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akawaponyesha watu wengi wenye magonjwa mbalimbali. Vilevile alifukuza pepo wengi, wala hakuwaachilia pepo kusema neno, kwa sababu walimujua yeye ni nani.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akaponya wengi waliokuwa na maradhi nyingine nyingine, akafukuza pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu walimjua.