Mark 1:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yohane Mbatizaji alitokea jangwani, akahubiri kwamba watu watubu na kubatizwa ili Mungu awasamehe dhambi zao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yahya alikuja akibatiza huko nyikani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yohana alitokea, akibatiza nyikani, na kuuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Naye Yohana akaja, akiwabatiza watu huko nyikani huku akiwahubiri watu ujumbe kutoka kwa Mungu. Aliwaambia wabatizwe kuonesha kuwa wamekubali kubadili maisha yao ndipo dhambi zao zitasamehewa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yohane Mbatizaji alitokea jangwani, akahubiri kwamba ni lazima watu watubu na kubatizwa ili Mungu awasamehe dhambi zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yohane Mbatizaji alitokea jangwani, akahubiri kwamba watu watubu na kubatizwa ili Mungu awasamehe dhambi zao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yohana alikuja, akibatiza huko nyikani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya ondoleo la dhambi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yahya alikuja, akibatiza huko nyikani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yohana alitokea akibatiza nyikani, na kuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yohane Mbatizaji alitokea jangwani, akahubiri kwamba watu watubu na kubatizwa ili Mungu awasamehe dhambi zao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yohana Mbatizaji alikuwa nyikani akibatiza na kutangaza ubatizo wa kujutisha, wapate kuondolewa makosa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yohana alitokea, akibatiza nyikani, na kuuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivi Yoane alitokea katika jangwa, akibatiza watu, akiwahubiri kwamba wageuke toka zambi zao, wabatizwe, na Mungu atawasamehe.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akatokea Yohana, akibatiza jangwani, na kuukhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi.