Mark 1:41 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akamwonea huruma, akanyosha mkono wake, akamgusa na kumwambia, “Nataka! Takasika!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa, akiwa amejawa na huruma, akaunyoosha mkono wake akamgusa, akamwambia, “Nataka. Takasika!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye akamhurumia, akanyosha mkono wake, akamgusa, akamwambia, Nataka, takasika.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Aliposikia maneno hayo Yesu akakasirika. Lakini akamhurumia. Akautoa mkono wake na kumgusa mtu yule mwenye ugonjwa mbaya sana wa ngozi, na kumwambia, “Ninataka kukuponya. Upone!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akamwonea huruma, akanyosha mkono wake, akamgusa na kumwambia, “Nataka, takasika!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akamwonea huruma, akanyosha mkono wake, akamgusa na kumwambia, “Nataka! Takasika!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akiwa amejawa na huruma, akanyosha mkono wake akamgusa, akamwambia, “Nataka takasika!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa, akiwa amejawa na huruma, akanyoosha mkono wake akamgusa, akamwambia, “Nataka. Takasika!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye akamhurumia, akanyosha mkono wake, akamgusa, akamwambia, Nataka, takasika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akamwonea huruma, akanyosha mkono wake, akamgusa na kumwambia, “Nataka! Takasika!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, alipomwonea uchungu, akanyosha mkono, akamgusa, akamwambia: Nataka, utakaswe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye akamhurumia, akanyosha mkono wake, akamgusa, akamwambia, Nataka, takasika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akamusikilia huruma, akanyoosha mukono, akamugusa na kumwambia: “Ninataka utakaswe!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu akamhurumia, akanyosha mkono wake, akamgusa, akamwambia, Nataka, takasika.