Mark 1:45 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini huyo mtu akaenda, akaanza kueneza habari hiyo kila mahali na kusema mambo mengi hata Yesu hakuweza tena kuingia katika mji wowote waziwazi; ikamlazimu kukaa nje, mahali pa faragha. Hata hivyo, watu wakamwendea kutoka kila upande.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini yule mtu akaenda akaanza kutangaza habari za kuponywa kwake waziwazi. Kwa hiyo, Isa hakuweza tena kuingia katika miji waziwazi bali alikaa sehemu zisizo na watu. Hata hivyo watu wakamfuata huko kutoka kila upande.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini akatoka, akaanza kuhubiri maneno mengi, na kulitangaza lile neno, hata Yesu asiweze tena kuingia mjini kwa wazi; bali alikuwako nje mahali pasipokuwa na watu, wakamwendea kutoka kila mahali.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini mtu yule aliondoka hapo na kwenda zake, na huko alianza kuzungumza kwa uhuru kamili na kusambaza habari hizo. Matokeo yake ni kwamba Yesu asingeweza tena kuingia katika mji kwa wazi wazi. Ikamlazimu kukaa mahali ambapo hakuna watu. Hata hivyo watu walikuja toka miji yote na kumwendea huko.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini huyo mtu akaenda, akaanza kueneza habari hiyo kila mahali na kusema mambo mengi hata Yesu hakuweza tena kuingia katika mji wowote waziwazi; ikamlazimu kukaa nje, mahali pa faragha. Hata hivyo, watu wakamwendea kutoka kila upande.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini huyo mtu akaenda, akaanza kueneza habari hiyo kila mahali na kusema mambo mengi hata Yesu hakuweza tena kuingia katika mji wowote waziwazi; ikamlazimu kukaa nje, mahali pa faragha. Hata hivyo, watu wakamwendea kutoka kila upande.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini yule mtu akaenda akaanza kutangaza habari za kuponywa kwake waziwazi. Kwa hiyo Yesu hakuweza tena kuingia katika miji waziwazi isipokuwa alikaa sehemu zisizo na watu. Lakini bado watu wakamfuata huko kutoka kila upande.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini yule mtu akaenda akaanza kutangaza habari za kuponywa kwake waziwazi. Kwa hiyo, Isa hakuweza tena kuingia katika miji waziwazi lakini alikaa sehemu zisizo na watu. Hata hivyo watu wakamfuata huko kutoka kila upande.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini akatoka, akaanza kuhubiri maneno mengi, na kulitangaza lile neno, hata Yesu asiweze tena kuingia mjini waziwazi; bali alikaa nje mahali pasipokuwa na watu, wakamwendea kutoka kila upande.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini huyo mtu akaenda, akaanza kueneza habari hiyo kila mahali na kusema mambo mengi hata Yesu hakuweza tena kuingia katika mji wowote waziwazi; ikamlazimu kukaa nje, mahali pa faragha. Hata hivyo, watu wakamwendea kutoka kila upande.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini alipotoka akaanza kutangaza mengi na kulisimulia jambo hilo po pote. Kwa hiyo Yesu hakuweza tena kuingia mjini waziwazi, ila alikuwa akikaa nje mahali palipokuwa pasipo watu, lakini watu wakamwendea toka pande zote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini akatoka, akaanza kuhubiri maneno mengi, na kulitangaza lile neno, hata Yesu asiweze tena kuingia mjini kwa wazi; bali alikuwako nje mahali pasipokuwa na watu, wakamwendea kutoka kila mahali.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mutu yule alipoenda, akaanza kutangaza habari zile fasi zote. Na kwa sababu hii Yesu hakuweza kuingia tena waziwazi katika muji wowote, lakini alibaki mbali nayo pahali penye ukiwa. Na watu walimufikia kule kutoka pande zote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nae akatoka, akaanza kukhubiri mengi, na kulitangaza lile neno, hatta Yesu asiweze tena kuingia mjini kwa wazi; bali alikuwa nje mabali pasipo watu; wakamwendea kutoka killa pahali.