Mark 10:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu alitoka hapo akaenda mkoani Yudea, hata ngambo ya mto Yordani. Umati wa watu ukamwendea tena, naye akawafundisha tena kama ilivyokuwa desturi yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akaondoka huko, akavuka Mto Yordani, akaenda sehemu za Yudea. Umati mkubwa wa watu wakaenda kwake tena, naye akawafundisha, kama ilivyokuwa desturi yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaondoka huko akafika mipakani mwa Uyahudi, na ng'ambo ya Yordani; makutano mengi wakakutanika tena wakamwendea; akawafundisha tena kama alivyozoea.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Naye aliondoka mahali pale, na kufika katika nchi ya Uyahudi ng'ambo ya Mto Yordani. Na makundi ya watu wakamjia tena na kama alivyofanya daima aliwafundisha.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alitoka hapo akaenda mkoani Yudea na hata ng'ambo ya mto Yordani. Umati wa watu ukamwendea tena, naye akawafundisha tena kama ilivyokuwa desturi yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu alitoka hapo akaenda mkoani Yudea, hata ng'ambo ya mto Yordani. Umati wa watu ukamwendea tena, naye akawafundisha tena kama ilivyokuwa desturi yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akaondoka huko akavuka Mto wa Yordani, akaenda sehemu ya Uyahudi. Umati mkubwa wa watu ukamjia tena na kama ilivyokuwa desturi yake akawafundisha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akaondoka huko, akavuka Mto Yordani, akaenda sehemu za Uyahudi. Umati mkubwa wa watu ukaenda kwake tena, naye kama ilivyokuwa desturi yake, akawafundisha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaondoka huko akafika katika eneo la Yudea, na ng'ambo ya Yordani; makutano mengi wakakutanika tena wakamwendea; akawafundisha tena kama alivyozoea.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu alitoka hapo akaenda mkoani Yudea, hata ngambo ya mto Yordani. Umati wa watu ukamwendea tena, naye akawafundisha tena kama ilivyokuwa desturi yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaondoka huko, akaja mipakani kwa Yudea na ng'ambo ya Yordani. Walipomkusanyikia tena makundi ya watu, akawafundisha tena, kama alivyozoea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaondoka huko akafika mipakani mwa Uyahudi, na ng’ambo ya Yordani; makutano mengi wakakutanika tena wakamwendea; akawafundisha tena kama alivyozoea.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akaondoka kule, akaenda katika jimbo la Yudea na kuvuka ngambo ingine ya Yordani. Na makundi mengi ya watu wakakusanyika tena mbele yake, naye akaanza kuwafundisha, kama vile alivyozoea kufanya.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
AKAONDOKA huko akafika mipaka ya Yahudi kwa niia ya ngʼambu ya Yardani; watu wengi wakakutanika tena wakamwendea; akawafundisha tena kama alivyozoea.