Mark 10:17 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu alipoanza tena safari yake, mtu mmoja alimjia mbio, akapiga magoti mbele yake, akamwuliza, “Mwalimu mwema, nifanyeje niupate uhai wa milele?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa alipokuwa anaondoka, mtu mmoja akamkimbilia, akapiga magoti mbele yake, akamuuliza, “Mwalimu mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na alipokuwa ameanza safari, mtu mmoja alimkimbilia, akafika na kupiga magoti mbele yake, akamwuliza, “Mwalimu mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alipoanza tena safari yake, mtu mmoja alimjia mbio, akapiga magoti mbele yake, akamwuliza, “Mwalimu mwema, nifanyeje ili niupate uzima wa milele?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu alipoanza tena safari yake, mtu mmoja alimjia mbio, akapiga magoti mbele yake, akamwuliza, “Mwalimu mwema, nifanyeje niupate uhai wa milele?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu alipokuwa anaondoka, mtu mmoja akamkimbilia, akapiga magoti mbele yake, akamwuliza, “Mwalimu mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa alipokuwa anaondoka, mtu mmoja akamkimbilia, akapiga magoti mbele yake, akamuuliza, “Mwalimu mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu alipoanza tena safari yake, mtu mmoja alimjia mbio, akapiga magoti mbele yake, akamwuliza, “Mwalimu mwema, nifanyeje niupate uhai wa milele?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Alipotoka na kufika njiani, mmoja akamjia mbio, akampigia magoti, akamwuliza: Mfunzi mwema, nifanye nini, niurithi uzima wa kale na kale?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu alipoondoka kwa kuendelea na safari yake, mutu mumoja akamufikia mbio akapiga magoti mbele yake na kumwuliza: “Mwalimu mwema, nifanye nini kusudi nipate kurizi uzima wa milele?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta alipokuwa akitoka kwenda njiani mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanyeni nipate kuurithi uzima wa milele?