Mark 10:21 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akamtazama, akampenda, akamwambia, “Umepungukiwa na kitu kimoja: Nenda ukauze kila kitu ulicho nacho, uwape maskini hizo fedha, nawe utakuwa na hazina mbinguni, kisha uje unifuate.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akamtazama na kumpenda, akamwambia, “Umepungukiwa na kitu kimoja. Nenda ukauze kila kitu ulicho nacho uwape maskini hizo fedha, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akamwangalia. Naye akashikwa na upendo kwa mtu yule, na hivyo akamwambia, “umekosa kitu kimoja: Nenda ukaviuze vyote ulivyo navyo kisha ukawape walio maskini, nawe utakuwa umejitunzia hazina mbinguni. Kisha uje ukanifuate.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akamtazama, akampenda, akamwambia, “Umepungukiwa na kitu kimoja: nenda ukauze vitu ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akamtazama, akampenda, akamwambia, “Umepungukiwa na kitu kimoja: nenda ukauze kila kitu ulicho nacho, uwape maskini hizo fedha, nawe utakuwa na hazina mbinguni, kisha uje unifuate.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akamtazama na kumpenda, akamwambia, “Umepungukiwa na kitu kimoja, nenda ukauze kila kitu ulicho nacho uwape maskini hizo fedha, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akamtazama na kumpenda, akamwambia, “Umepungukiwa na kitu kimoja. Nenda ukauze kila kitu ulicho nacho uwape maskini hizo fedha, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Nenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akamtazama, akampenda, akamwambia, “Umepungukiwa na kitu kimoja: Nenda ukauze kila kitu ulicho nacho, uwape maskini hizo fedha, nawe utakuwa na hazina mbinguni, kisha uje unifuate.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yesu akamtazama, akampenda, akamwambia: Umesaza kimoja: nenda, uviuze vyote, ulivyo navyo, uvigawie maskini! Hivyo utakuwa na kilimbiko mbinguni. Kisha uje, ujitwishe msalaba wako, unifuate!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akamwangalia kwa upendo, akamwambia: “Unakosewa na kitu kimoja tu: kwenda uuzishe vitu vyote unavyokuwa navyo, na uwape wamasikini mali zile, nawe utakuwa na akiba mbinguni. Kisha urudi, unifuate!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa neno moja Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni: ukiisha, njoo ukajitwike msalaba wako unifuate.