Mark 10:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akatazama pande zote, akawaambia wanafunzi wake, “Jinsi gani itakavyokuwa vigumu kwa matajiri kuingia katika ufalme wa Mungu!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akatazama pande zote, akawaambia wanafunzi wake, “Itakuwa vigumu sana kwa wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Jinsi itakavyokuwa shida wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu!
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu aligeuka kuwatazama wanafunzi wake na kuwaambia wake, “Angalieni jinsi ilivyo vigumu sana kwa walio na mali nyingi kuingia katika ufalme wa Mungu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akatazama pande zote, akawaambia wanafunzi wake, “Jinsi gani itakavyokuwa vigumu kwa matajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akatazama pande zote, akawaambia wanafunzi wake, “Jinsi gani itakavyokuwa vigumu kwa matajiri kuingia katika ufalme wa Mungu!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akatazama pande zote, akawaambia wanafunzi wake, “Itakuwa vigumu sana kwa wenye mali kuingia kwenye Ufalme wa Mungu!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akatazama pande zote, akawaambia wanafunzi wake, “Itakuwa vigumu sana kwa wenye mali kuingia katika Ufalme wa Mwenyezi Mungu!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Jinsi itakavyokuwa shida wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akatazama pande zote, akawaambia wanafunzi wake, “Jinsi gani itakavyokuwa vigumu kwa matajiri kuingia katika ufalme wa Mungu!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Yesu akatazama huko na huko, akawaambia wanafunzi wake: Vitazameni vigumu vinavyowazuia waegemeao mali kuingia katika ufalme wa Mungu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Jinsi itakavyokuwa shida wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akaangalia pande zake zote na kuwaambia wanafunzi wake: “Kweli ni vigumu sana kwa watajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Kwa shidda gani wenye mali wataingia katika ufalme wa Mungu!