Mark 10:24 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wanafunzi walishangazwa na maneno yake. Yesu akawaambia tena, “Watoto wangu, ni vigumu sana kuingia katika ufalme wa Mungu!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanafunzi wake wakashangazwa sana na maneno hayo. Lakini Isa akawaambia tena, “Wanangu, tazama jinsi ilivyo vigumu kwa wale wanaotumainia mali kuingia katika ufalme wa Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake. Yesu akajibu tena, akawaambia, Watoto, jinsi ilivyo shida wenye kutegemea mali kuingia katika ufalme wa Mungu!
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wanafunzi wake walistaajabishwa na maneno yale. Lakini Yesu akawaambia tena, “Wanangu, ni vigumu sana kuuingia ufalme wa Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wanafunzi walishangazwa na maneno yake. Yesu akawaambia tena, “Watoto wangu, ni vigumu sana kuingia katika Ufalme wa Mungu!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wanafunzi walishangazwa na maneno yake. Yesu akawaambia tena, “Watoto wangu, ni vigumu sana kuingia katika ufalme wa Mungu!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wanafunzi wake wakashangazwa sana na maneno hayo. Lakini Yesu akawaambia tena, “Wanangu, tazama jinsi ilivyo vigumu kwa wale wanaotumainia mali kuingia katika Ufalme wa Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wanafunzi wake wakashangazwa sana na maneno hayo. Lakini Isa akawaambia tena, “Wanangu, tazama jinsi ilivyo vigumu kwa wale wanaotumainia mali kuingia katika Ufalme wa Mwenyezi Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake. Yesu akajibu tena, akawaambia, Watoto, jinsi ilivyo shida wenye kutegemea mali kuingia katika ufalme wa Mungu!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wanafunzi walishangazwa na maneno yake. Yesu akawaambia tena, “Watoto wangu, ni vigumu sana kuingia katika ufalme wa Mungu!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wanafunzi walipoingiwa na kituko kwa hayo mnaneno yake, Yesu akajibu, akawaambia tena: Wanangu, vitazameni vigumu vinavyozuia kuingia katika ufalme wa Mungu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake. Yesu akajibu tena, akawaambia, Watoto, jinsi ilivyo shida wenye kutegemea mali kuingia katika ufalme wa Mungu!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanafunzi wakashangaa sana kusikia maneno hayo. Lakini Yesu akawaambia tena: “Watoto wangu, ni vigumu kabisa kuingia katika Ufalme wa Mungu!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake. Yesu akajibu tena, akawaambia, Watoto, kwa shidda gani wenye kuitegemea mali wataingia katika ufalme wa Mungu!