Mark 10:32 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, walikuwa njiani kwenda juu Yerusalemu, na Yesu alikuwa anawatangulia. Wanafunzi wake walijawa na hofu, na watu waliofuata waliogopa. Yesu akawachukua tena kando wale kumi na wawili, akaanza kuwaambia yale yatakayompata:
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walikuwa njiani wakipanda kwenda Yerusalemu, na Isa alikuwa amewatangulia. Wanafunzi wake walishangaa, nao watu waliowafuata walijawa na hofu. Isa akawachukua tena wale wanafunzi wake kumi na wawili kando na kuwaambia yatakayompata.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao walikuwako njiani, huku wakipanda kwenda Yerusalemu; na Yesu alikuwa akiwatangulia, wakashangaa, nao katika kufuata wakaogopa. Akawatwaa tena wale Thenashara, akaanza kuwaambia habari za mambo yatakayompata,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Walikuwa wote njiani wakipanda kuelekea Yerusalemu, na Yesu alikuwa akitembea mbele yao. Nao walisumbuka sana. Na wale waliowafuata walikuwa na hofu pia. Kwa mara nyingine Yesu akawachukua wale wanafunzi kumi na mbili pembeni, na akaanza kuwaeleza yale yatakayomtokea Yerusalemu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, walikuwa njiani kwenda Yerusalemu, na Yesu alikuwa anawatangulia. Wanafunzi wake walijawa na hofu, na watu waliofuata waliogopa. Yesu akawachukua tena kando wale kumi na wawili, akaanza kuwaambia yale yatakayompata:
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, walikuwa njiani kwenda juu Yerusalemu, na Yesu alikuwa anawatangulia. Wanafunzi wake walijawa na hofu, na watu waliofuata waliogopa. Yesu akawachukua tena kando wale kumi na wawili, akaanza kuwaambia yale yatakayompata:
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walikuwa njiani wakipanda kwenda Yerusalemu na Yesu alikuwa ametangulia. Wanafunzi wake walishangaa, nao watu waliowafuata walijawa na hofu. Yesu akawachukua tena wale wanafunzi wake kumi na wawili kando na kuwaambia yatakayompata.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walikuwa njiani wakipanda kwenda Yerusalemu, na Isa alikuwa ametangulia. Wanafunzi wake walishangaa, nao watu waliowafuata walijawa na hofu. Isa akawachukua tena wale wanafunzi wake kumi na wawili kando na kuwaambia yatakayompata.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao walikuwako njiani, huku wakipanda kwenda Yerusalemu; na Yesu alikuwa akiwatangulia, wakashangaa, nao katika kufuata wakaogopa. Akawatwaa tena wale Kumi na Wawili, akaanza kuwaambia kuhusu mambo yatakayompata,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, walikuwa njiani kwenda juu Yerusalemu, na Yesu alikuwa anawatangulia. Wanafunzi wake walijawa na hofu, na watu waliofuata waliogopa. Yesu akawachukua tena kando wale kumi na wawili, akaanza kuwaambia yale yatakayompata:
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipokuwa njiani wakipanda kwenda Yerusalemu, Yesu alikuwa anatangulia mbele yao. Nao wakashikwa na kituko, wakamfuata na kuogopa. Akawachukua tena wale kumi na wawili, akaanza kuwaambia mambo yatakayompata,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao walikuwako njiani, huku wakipanda kwenda Yerusalemu; na Yesu alikuwa akiwatangulia, wakashangaa, nao katika kufuata wakaogopa. Akawatwaa tena wale Thenashara, akaanza kuwaambia habari za mambo yatakayompata,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu na wanafunzi wake walipokuwa katika njia, wakipanda kwenda Yerusalema, yeye akatangulia mbele yao. Wanafunzi walishikwa na hofu, nao watu waliowafuata waliogopa. Yesu akawatwaa tena wanafunzi wake kumi na wawili, na kuanza kusemezana nao juu ya mambo yatakayomupata.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakawa njiani, wakipanda kwenda Yerusalemi; na Yesu alikuwa akiwatangulia: wakashangaa, na wakifuata wakaogopa. Akawachukua tena wale thenashara akaanza kuwaambia khabari za mambo yatakayompata, akinena,