Mark 10:40 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini ni nani atakayeketi kulia au kushoto kwangu si wajibu wangu kupanga bali nafasi hizo watapewa wale waliotayarishiwa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
lakini kuketi mkono wangu wa kuume au wa kushoto si juu yangu mimi kuwapa. Nafasi hizi ni kwa ajili ya wale walioandaliwa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
lakini habari ya kuketi mkono wangu wa kuume au mkono wangu wa kushoto si langu kuwapa, ila wao watapewa waliowekewa tayari.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini kuhusu kuketi kulia kwangu ama kushoto kwangu siyo mamlaka yangu kusema. Mungu ameandaa nafasi hizo kwa ajili ya wale aliowateuwa.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini ni nani atakayeketi kulia au kushoto kwangu si wajibu wangu kupanga, bali nafasi hizo watapewa wale waliotayarishiwa.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini ni nani atakayeketi kulia au kushoto kwangu si wajibu wangu kupanga bali nafasi hizo watapewa wale waliotayarishiwa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
lakini kuketi mkono wangu wa kuume au wa kushoto si juu yangu mimi kuwapa. Nafasi hizi ni kwa ajili ya wale walioandaliwa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
lakini kuketi mkono wangu wa kuume au wa kushoto si juu yangu mimi kuwapa. Nafasi hizi ni kwa ajili ya wale walioandaliwa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
lakini kuhusu kuketi katika mkono wangu wa kulia au mkono wangu wa kushoto si langu kuwapa, ila wao watapewa waliowekewa tayari.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini ni nani atakayeketi kulia au kushoto kwangu si wajibu wangu kupanga bali nafasi hizo watapewa wale waliotayarishiwa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
lakini kumketisha mtu kuumeni au kushotoni kwangu hii si kazi yangu, ila hupewa walioandaliwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
lakini habari ya kuketi mkono wangu wa kuume au mkono wangu wa kushoto si langu kuwapa, ila wao watapewa waliowekewa tayari.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kuikalisha mutu kwa upande wangu wa kuume au wa kushoto si kazi yangu. Ni Mungu peke yake atakayeweka watu aliowatayarisha kwenye nafasi zile.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
bali khabari ya kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto sina amri kuwapeni, illa wao watapewa waliowekewa tayari.