Mark 10:42 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo, Yesu akawaita, akawaambia, “Mnajua kwamba wale wanaofikiriwa kuwa watawala wa mataifa huwatawala watu wao kwa mabavu, na wakuu hao huwamiliki watu wao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Isa akawaita wote pamoja na kuwaambia, “Mnafahamu kuwa wale wanaodhaniwa kuwa watawala wa watu wa Mataifa huwatawala watu kwa nguvu, nao wenye vyeo huonesha mamlaka yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yesu akawaita, akawaambia, Mwajua ya kuwa wale wanaohesabiwa kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na Yesu akawaita wale wanafunzi kumi na kusema, “Mnajua kuwa miongoni mwa mataifa watawala huwa na mamlaka makubwa juu ya watu, na viongozi wenye nguvu huwakandamiza watu wao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akawaita, akawaambia, “Mnajua kwamba wale wanaofikiriwa kuwa watawala wa mataifa huwatawala watu wao kwa mabavu, na wakuu hao huwamiliki watu wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo, Yesu akawaita, akawaambia, “Mnajua kwamba wale wanaofikiriwa kuwa watawala wa mataifa huwatawala watu wao kwa mabavu, na wakuu hao huwamiliki watu wao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akawaita wanafunzi wake pamoja akawaambia, “Mnafahamu kuwa watawala wa watu Mataifa huwatawala watu kwa nguvu, nao wenye vyeo huwaonyesha mamlaka yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Isa akawaita wote pamoja na kuwaambia, “Mnafahamu kuwa wale wanaodhaniwa kuwa watawala wa watu wa Mataifa huwatawala watu kwa nguvu, nao wenye vyeo huonyesha mamlaka yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu akawaita, akawaambia, Mwajua ya kuwa wale wanaohesabiwa kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo, Yesu akawaita, akawaambia, “Mnajua kwamba wale wanaofikiriwa kuwa watawala wa mataifa huwatawala watu wao kwa mabavu, na wakuu hao huwamiliki watu wao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yesu akawaita, wamjongelee, akawaambia: Mnajua: wanaotazamwa kuwa wafalme wa mataifa huwatawala, nao wakubwa wao huwatumikisha kwa nguvu. Kwenu ninyi visiwe hivyo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yesu akawaita, akawaambia, Mwajua ya kuwa wale wanaohesabiwa kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akawaita wote na kuwaambia: “Munajua kwamba wale wanaohesabiwa kuwa watawala wa mataifa wanayatawala kwa kinguvu, na wakubwa yao wanayagandamiza.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu akawaita, akawaambia, Mwajua ya kuwa wale wanaohesabiwa kuwa majumbe wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha.