Mark 10:45 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana Mwana wa Mtu hakuja kutumikiwa, ila kutumikia, na kutoa maisha yake kuwa fidia ya watu wengi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa hata Mwana wa Adamu hakuja ili kutumikiwa, bali kutumika na kuutoa uhai wake uwe fidia kwa ajili ya wengi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwani hata Mwana wa Adamu hakuja ili kutumikiwa bali alikuja kuwatumikia wengine na kuyatoa maisha yake ili kuwaweka huru wengi.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana Mwana wa Mtu hakuja kutumikiwa, ila alikuja kutumikia, na kutoa maisha yake kuwa fidia ya watu wengi.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana Mwana wa Mtu hakuja kutumikiwa, ila kutumikia, na kutoa maisha yake kuwa fidia ya watu wengi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa hata Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa, bali kutumika na kuutoa uhai wake kuwa ukombozi kwa ajili ya wengi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa hata Mwana wa Adamu hakuja ili kutumikiwa, bali kutumika na kuutoa uhai wake uwe fidia kwa ajili ya wengi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana Mwana wa Mtu hakuja kutumikiwa, ila kutumikia, na kutoa maisha yake kuwa fidia ya watu wengi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani naye Mwana wa mtu hakuja, atumikiwe, ila amekuja kutumika na kuitoa roho yake kuwa makombozi ya watu wengi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana hata Mwana wa Mutu hakuja kutumikiwa, lakini kutumika na kutoa maisha yake kusudi awakomboe watu wengi.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana Mwana wa Adamu nae hakuja kukhudumiwa bali kukhudumu, na kutoa roho yake iwe dia ya wengi.