Mark 10:49 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu alisimama, akasema, “Mwiteni.” Basi, wakamwita huyo kipofu, wakamwambia, “Jipe moyo! Simama, anakuita.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akasimama na kusema, “Mwiteni.” Hivyo wakamwita yule mtu kipofu, wakamwambia, “Jipe moyo! Inuka, anakuita.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yesu akasimama akasema, Mwiteni. Wakamwita yule kipofu, wakamwambia, Jipe moyo; inuka, anakuita.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa hiyo Yesu akasimama na kusema, “Hebu mwiteni.” Nao wakamwita yule mtu asiyeona na kumweleza, “Jipe moyo mkuu! Inuka! Yesu anakuita.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alisimama, akasema, “Mwiteni.” Basi, wakamwita huyo kipofu, wakamwambia, “Jipe moyo! Simama, anakuita.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu alisimama, akasema, “Mwiteni.” Basi, wakamwita huyo kipofu, wakamwambia, “Jipe moyo! Simama, anakuita.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akasimama na kusema, “Mwiteni.” Hivyo wakamwita yule mtu kipofu wakamwambia, “Jipe moyo! Inuka, anakuita.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akasimama na kusema, “Mwiteni.” Hivyo wakamwita yule mtu kipofu, wakamwambia, “Jipe moyo! Inuka, anakuita.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu akasimama akasema, Mwiteni. Wakamwita yule kipofu, wakamwambia, Jipe moyo; inuka, anakuita.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu alisimama, akasema, “Mwiteni.” Basi, wakamwita huyo kipofu, wakamwambia, “Jipe moyo! Simama, anakuita.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Yesu aliposimama, akasema: Mwiteni! Wakamwita kipofu, wakamwambia: Tulia moyo, inuka! anakuita.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yesu akasimama akasema, Mwiteni. Wakamwita yule kipofu, wakamwambia, Jipe moyo; inuka, anakuita.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akasimama na kusema: “Mumwite.” Basi wakamwita yule kipofu na kumwambia: “Ujipe moyo! Simama, anakuita.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakamwita yule kipofu, wakamwambia, Jipe moyo; ondoka, anakuita.