Mark 11:13 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, akaona kwa mbali mtini wenye majani mengi. Akauendea ili aone kama ulikuwa na tunda lolote. Alipoufikia, aliukuta bila tunda lolote ila tu majani matupu, kwa vile hayakuwa majira yake ya matunda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akauona mtini kwa mbali, naye akaenda ili aone kama ulikuwa na matunda. Alipoufikia, akakuta una majani tu, kwa kuwa hayakuwa majira ya tini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili labda aone kitu juu yake; na alipoufikilia hakuona kitu ila majani; maana si wakati wa tini.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na kutokea mbali akauona mti wa mtini umefunikwa kwa matawi yake mengi, hivyo akausogelea karibu ili kuona kama atakuta tunda lolote juu yake. Lakini alipoufikia hakukuta tunda lolote isipokuwa matawi tu kwani hayakuwa majira ya mitini kuwepo katika mti.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, akaona kwa mbali mtini wenye majani mengi. Akauendea ili aone kama ulikuwa na tunda lolote. Alipoufikia, aliukuta bila tunda lolote ila majani matupu, kwa vile hayakuwa majira ya mtini kuzaa matunda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, akaona kwa mbali mtini wenye majani mengi. Akauendea ili aone kama ulikuwa na tunda lolote. Alipoufikia, aliukuta bila tunda lolote ila tu majani matupu, kwa vile hayakuwa majira yake ya matunda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipouona mtini kwa mbali, akaenda ili aone kama ulikuwa na matunda. Alipoufikia, akakuta una majani tu, kwa kuwa hayakuwa majira ya tini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akauona mtini kwa mbali, naye akaenda ili aone kama ulikuwa na matunda. Alipoufikia, akakuta una majani tu, kwa kuwa hayakuwa majira ya tini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili labda aone kitu juu yake; na alipoufikia hakuona kitu ila majani; maana si wakati wa tini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, akaona kwa mbali mtini wenye majani mengi. Akauendea ili aone kama ulikuwa na tunda lolote. Alipoufikia, aliukuta bila tunda lolote ila tu majani matupu, kwa vile hayakuwa majira yake ya matunda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huko mbali akaona mkuyu wenye majani, akaenda, aone, kama liko tunda juu yake. Akaufikia, asione kitu, ila majani tu, kwani siku za kuyu hazijawa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili labda aone kitu juu yake; na alipoufikilia hakuona kitu ila majani; maana si wakati wa tini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akaona kwa mbali muti wa tini wenye majani mengi. Basi akaenda kuangalia kama atapata matunda juu ya muti ule. Lakini alipofika karibu nao, hakuona kitu juu yake isipokuwa majani matupu, kwa sababu haikukuwa wakati wake wa kutoa matunda.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akaona toka mbali mtini wenye majani, akaenda illi labuda aone kitu juu yake: na alipofika hakuona kitu illa majani: