Mark 11:14 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo akauambia mtini, “Tangu leo hata milele mtu yeyote asile matunda kwako.” Nao wanafunzi wake walisikia maneno hayo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akauambia ule mti, “Tangu leo mtu yeyote asile kamwe matunda kutoka kwako.” Wanafunzi wake walimsikia akisema hayo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akajibu, akauambia, Tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Akauambia mtini ule, “Mtu yeyote asile matunda kutoka kwako kamwe milele!” Na wanafunzi wake waliyasikia hayo maneno.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo akauambia mtini, “Tangu leo hata milele mtu yeyote asile matunda kwako.” Nao wanafunzi wake walisikia maneno hayo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo akauambia mtini, “Tangu leo hata milele mtu yeyote asile matunda kwako.” Nao wanafunzi wake walisikia maneno hayo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akauambia ule mti, “Tangu leo mtu ye yote na asile kamwe matunda kutoka kwako.” Wanafunzi wake walimsikia akisema hayo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akauambia ule mti, “Tangu leo mtu yeyote asile kamwe matunda kutoka kwako.” Wanafunzi wake walimsikia akisema hayo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akajibu, akauambia, Tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo akauambia mtini, “Tangu leo hata milele mtu yeyote asile matunda kwako.” Nao wanafunzi wake walisikia maneno hayo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, alipotoa neno la kwamba: Kale na kale mtu asile tena kwako tunda! Wanafunzi wake wakayasikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akajibu, akauambia, Tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Yesu akalaani muti ule, akisema: “Tangia sasa hata milele, mutu asipate tena tunda tokea juu yako.” Nao wanafunzi wake wakasikia maneno hayo aliyosema.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
maana haukuwa wakati wa tini. Yesu akajibu, akauambia, Tangu leo hatta milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia.