Mark 11:17 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha akawafundisha, “Imeandikwa: ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa ajili ya mataifa yote!’ Lakini nyinyi mmeifanya kuwa pango la wanyanganyi!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye alipokuwa akiwafundisha, akasema, “Je, haikuandikwa kuwa: “ ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote’? Lakini ninyi mmeifanya kuwa ‘pango la wanyang’anyi.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akafundisha, akasema, Je! Haikuandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akaanza kuwafundisha na kuwaeleza, “Je, haikuandikwa katika Maandiko kwamba: ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ambapo watu wa mataifa yote wataleta maombi yao kwangu’? Lakini ninyi mmeifanya kuwa ‘mahali pa wezi kujificha.’ ”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha akawafundisha, “Imeandikwa: Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa ajili ya mataifa yote! Lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha akawafundisha, “Imeandikwa: ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa ajili ya mataifa yote!’ Lakini nyinyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye alipokuwa akiwafundisha, akasema, “Je, haikuandikwa kuwa: “ ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote’? Lakini ninyi mmeifanya kuwa ‘pango la wanyang'anyi.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye alipokuwa akiwafundisha, akasema, “Je, haikuandikwa kuwa: “ ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote’? Lakini ninyi mmeifanya kuwa ‘pango la wanyang’anyi.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akafundisha, akasema, Je! Haikuandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha akawafundisha, “Imeandikwa: ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa ajili ya mataifa yote!’ Lakini nyinyi mmeifanya kuwa pango la wanyanganyi!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawafundisha akiwaambia: Haikuandikwa ya kuwa: Nyumba yangu itaitwa nyumba ya kuombea kwao makabila yote ya watu? Lakini ninyi mmeigeuza kuwa pango la wanyang'anyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akafundisha, akasema, Je! Haikuandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha akawafundisha maneno haya: “Imeandikwa katika Maandiko Matakatifu: ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya maombi kwa mataifa yote.’ Lakini ninyi mumeigeuza kuwa nafasi ya kukutania ya wanyanganyi!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akafundisha, akiwaambia, Haikuandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali nanyi mmeifanya kuwa pango ya wanyangʼanyi.