Mark 11:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
akawaambia, “Nendeni katika kijiji kilicho mbele yenu. Mtakapokuwa mnaingia humo, mtakuta mwanapunda amefungwa, ambaye bado hajatumiwa na mtu. Mfungueni mkamlete.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
akawaambia, “Nendeni katika kijiji kilicho mbele yenu. Na hapo mtakapoingia kijijini, mtampata mwana-punda amefungwa hapo, ambaye hajapandwa na mtu bado. Mfungueni, mkamlete hapa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akawaambia, Nendeni mpaka kile kijiji kinachowakabili; na katika kuingia ndani yake, mara mtaona mwana-punda amefungwa, asiyepandwa na mtu bado; mfungueni, kamleteni.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
na kuwaagiza, “Mwende katika kijiji kilichopo ngambo yenu kule, na mara tu mtakapoingia ndani yake mtakuta mwana punda amefungwa mahali na ambaye hajawahi kupandwa na mtu yeyote. Mfungueni na kisha mumlete hapa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
akawaambia, “Nendeni katika kijiji kilicho mbele yenu. Mtakapokuwa mnaingia humo, mtakuta mwana punda amefungwa ambaye bado hajatumiwa na mtu. Mfungueni mkamlete.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
akawaambia, “Nendeni katika kijiji kilicho mbele yenu. Mtakapokuwa mnaingia humo, mtakuta mwanapunda amefungwa, ambaye bado hajatumiwa na mtu. Mfungueni mkamlete.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
akiwaambia, “Nendeni kwenye kijiji kilichoko mbele yenu na mara mwingiapo kijijini, mtakuta mwana punda amefungwa, ambaye hajapandwa na mtu ye yote. Mfungueni, mkamlete hapa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
akawaambia, “Nendeni katika kijiji kilichoko mbele yenu. Na hapo mtakapoingia kijijini, mtamkuta mwana-punda amefungwa hapo, ambaye hajapandwa na mtu bado. Mfungueni, mkamlete hapa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akawaambia, Nendeni mpaka kile kijiji kinachowakabili; na katika kuingia ndani yake, mara mtaona mwanapunda amefungwa, asiyepandwa na mtu bado; mfungueni, kamleteni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
akawaambia, “Nendeni katika kijiji kilicho mbele yenu. Mtakapokuwa mnaingia humo, mtakuta mwanapunda amefungwa, ambaye bado hajatumiwa na mtu. Mfungueni mkamlete.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akawaambia: Nendeni katika kijiji kinachowaelekea! Mtakapoingia mle mara mtaona, pamefungwa mwana punda, ambaye mtu hajampanda bado; mfungueni, mmlete!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akawaambia, Nendeni mpaka kile kijiji kinachowakabili; na katika kuingia ndani yake, mara mtaona mwana-punda amefungwa, asiyepandwa na mtu bado; mfungueni, kamleteni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
akiwaambia: “Mwende katika kijiji kinachokuwa mbele yenu. Wakati mutakapofika kule, mutaona mwana-punda amefungwa, na hakuna mutu aliyekwisha kupanda juu yake. Mumufungue na kumuleta hapa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Enendeni zenu hatta kile kijiji kinachowakahili. Katika kuingia ndani yake marra mtaona mwana punda amefungwa, asiyepandwa na mtu hado; mfungueni, kamleteni.