Mark 11:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nawaambieni kweli, mtu akiuambia mlima huu: ‘Ngoka ukajitose baharini,’ bila kuona shaka moyoni mwake, ila akaamini kwamba mambo yote anayosema yanafanyika, atafanyiwa jambo hilo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Amin, nawaambia, mtu yeyote atakayeuambia mlima huu, ‘Ng’oka ukatupwe baharini,’ wala asione shaka moyoni mwake, bali aamini kwamba hayo asemayo yametukia, atatimiziwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nawaambia kweli: Yeyote atakayeuambia mlima huu, ‘Ng'oka na ukajitupe katika bahari’; kama asipokuwa na mashaka moyoni mwake, Lakini akaamini kuwa kile anachokisema kitatokea, huyo atatendewa hayo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nawaambieni kweli, mtu akiuambia mlima huu: Ng'oka ukajitose baharini bila kuona shaka moyoni mwake, ila akaamini kwamba mambo yote anayosema yanafanyika, atafanyiwa jambo hilo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nawaambieni kweli, mtu akiuambia mlima huu: ‘Ng'oka ukajitose baharini,’ bila kuona shaka moyoni mwake, ila akaamini kwamba mambo yote anayosema yanafanyika, atafanyiwa jambo hilo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Amin, amin nawaambia, mtu ye yote atakayeuambia mlima huu, ‘Ng'oka ukatupwe baharini,’ wala asione shaka moyoni mwake, bali aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Amin, nawaambia, mtu yeyote atakayeuambia mlima huu, ‘Ng’oka ukatupwe baharini,’ wala asione shaka moyoni mwake, bali aamini kwamba hayo asemayo yametukia, atatimiziwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Amin, nawaambia, yeyote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nawaambieni kweli, mtu akiuambia mlima huu: ‘Ngoka ukajitose baharini,’ bila kuona shaka moyoni mwake, ila akaamini kwamba mambo yote anayosema yanafanyika, atafanyiwa jambo hilo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kweli nawaambiani: Kila atakayeuambia mlima huu: Ondoka hapa, ulipo, ujitupe baharini! basi, litatimia vivyo hivyo, asipokuwa na mashaka moyoni mwake, ila akiwa anayategemea tu ya kuwa: Analolisema, litatendeka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kweli ninawaambia: ‘Mutu anaweza kuuambia mulima huu kwamba uondoke hapa na kujitupa katika bahari.’ Na ikiwa anasema maneno yale bila shaka katika moyo wake, lakini akiamini kama jambo lile litafanyika, hakika litafanyika kwake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Amin, nawaambieni, Ye yote atakaenambia mlima huu, Ngʼoka ukatupwe baharini, asione shaka moyoni mwake, bali aamini kwamba hayo asemayo yamekuwa, yatamtukia hayohayo aliyosema.