Mark 12:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu alianza kusema nao kwa mifano: “Mtu mmoja alilima shamba la mizabibu. Akalizungushia ukuta, na katikati yake akachimba kisima cha kusindikia divai, akajenga mnara pia. Akalikodisha shamba hilo kwa wakulima, akasafiri hadi nchi ya mbali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akaanza kusema nao kwa mifano, akawaambia: “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu. Akajenga ukuta kulizunguka, na ndani yake akachimba shimo la shinikizo la kukamulia zabibu, na akajenga mnara wa ulinzi. Kisha akalikodisha shamba hilo la mizabibu kwa wakulima fulani, kisha akasafiri hadi nchi nyingine.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaanza kusema nao kwa mifano; Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu, akazungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu alianza kuongea nao kwa simulizi zenye mafumbo: “Mtu mmoja alipanda mizabibu shambani. Akajenga ukuta kuizunguka, akachimba shimo kwa ajili ya kukamulia mizabibu na kisha alijenga mnara. Baadaye alilikodisha kwa baadhi ya wakulima na akaenda safari nchi ya mbali.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alianza kusema nao kwa mifano: “Mtu mmoja alilima shamba la mizabibu. Akalizungushia ukuta, na katikati yake akachimba kisima cha kusindikia divai, akajenga mnara pia. Akalikodisha shamba hilo kwa wakulima, akasafiri hadi nchi ya mbali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu alianza kusema nao kwa mifano: “Mtu mmoja alilima shamba la mizabibu. Akalizungushia ukuta, na katikati yake akachimba kisima cha kusindikia divai, akajenga mnara pia. Akalikodisha shamba hilo kwa wakulima, akasafiri hadi nchi ya mbali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akaanza kusema nao kwa mifano, akawaambia: “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu. Akajenga ukuta kulizunguka, akachimba shimo ndani yake kwa ajili ya shinikizo la kusindika divai, akajenga mnara wa ulinzi. Akalikodisha shamba hilo kwa wakulima, kisha akasafiri kwenda nchi nyingine.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akaanza kusema nao kwa mifano, akawaambia: “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu. Akajenga ukuta kulizunguka, akachimba shimo ndani yake kwa ajili ya shinikizo la kusindika divai, na akajenga mnara wa ulinzi. Kisha akalikodisha shamba hilo la mizabibu kwa wakulima fulani, kisha akasafiri kwenda nchi nyingine.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaanza kusema nao kwa mifano; Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu, akalizungushia ua, akachimba shimo la shinikizo, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu alianza kusema nao kwa mifano: “Mtu mmoja alilima shamba la mizabibu. Akalizungushia ukuta, na katikati yake akachimba kisima cha kusindikia divai, akajenga mnara pia. Akalikodisha shamba hilo kwa wakulima, akasafiri hadi nchi ya mbali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaanza kusema nao kwa mifano. Mtu alipanda mizabibu, akaizungusha ugo, akachimbua kamulio la kuzikamulia zabibu, ajenga dungu, akaipangisha wakulima, kisha akaenda katika nchi nyingine.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaanza kusema nao kwa mifano; Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu, akazungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Yesu akaanza kusema maneno haya kwa wale wakubwa kwa njia ya mifano: “Mutu mumoja alipanda shamba la mizabibu, akalizungusha na upango, akatengeneza nafasi ya kukamulia matunda ya mizabibu na kujenga munara kwa ajili ya walinzi wa shamba. Kisha akalipangisha kwa walimaji, akaenda safari katika inchi ingine.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
AKAANZA kusema nao kwa mifano. Mtu alipanda mizabibu, akazungusha nzio, akachimbia shimo lake shinikizo, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri.