Mark 12:14 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakamwendea, wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwaminifu unayesema ukweli mtupu, wala humjali mtu yeyote. Wala cheo cha mtu si kitu kwako, lakini wafundisha ukweli kuhusu njia ya Mungu. Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la? Tulipe au tusilipe?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakamjia, wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwadilifu. Wewe huyumbishwi na wanadamu, kwa kuwa huna upendeleo. Lakini wewe huifundisha njia ya Mungu katika kweli. Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata walipofika walimwambia, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, wala hujali cheo cha mtu; kwa maana hutazami sura za watu; lakini katika kweli waifundisha njia ya Mungu. Je! Ni halali kumpa Kaisari kodi au siyo?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wale waliotumwa walifika na kumwambia, “Mwalimu tunajua, kwamba wewe ni mkweli, na tena hujali yale watu wanayoyafikiri kuhusu wewe, kwa sababu wewe hubabaishwi na wadhifa wa mtu. Lakini unafundisha ukweli wa njia ya Mungu. Tuambie ni haki kulipa kodi kwa Kaisari ama la? Je, tulipe au tusilipe?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakamwendea, wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwaminifu unayesema ukweli mtupu, wala humjali mtu yeyote. Wala cheo cha mtu si kitu kwako, lakini wafundisha ukweli kuhusu njia ya Mungu. Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la? Tulipe au tusilipe?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakamwendea, wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwaminifu unayesema ukweli mtupu, wala humjali mtu yeyote. Wala cheo cha mtu si kitu kwako, lakini wafundisha ukweli kuhusu njia ya Mungu. Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la? Tulipe au tusilipe?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakamjia, wakamwambia, “Mwalimu, tunajua ya kuwa wewe ni mtu mwadilifu. Wewe huyumbishwi na wanadamu, kwa kuwa hujali kwamba wao ni nani. Lakini wewe hulifundisha neno la Mungu sawasawa na kweli. Je, ni haki kumlipa Kaisari kodi au la?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakamjia, wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwadilifu. Wewe huyumbishwi na wanadamu, kwa kuwa huna upendeleo. Lakini wewe huifundisha njia ya Mungu katika kweli. Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata walipofika walimwambia, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, wala hujali cheo cha mtu; kwa maana hutazami sura za watu; lakini katika kweli waifundisha njia ya Mungu. Je! Ni halali kumpa Kaisari kodi au siyo?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakamwendea, wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwaminifu unayesema ukweli mtupu, wala humjali mtu yeyote. Wala cheo cha mtu si kitu kwako, lakini wafundisha ukweli kuhusu njia ya Mungu. Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la? Tulipe au tusilipe?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakaja, wakamwambia: Mfunzi, tumekujua, ya kuwa wewe ni mtu wa kweli, tena humwuliziulizi mtu ye yote, kwani hutazami nyuso za watu, nayo njia ya Mungu unaifundisha, ilivyo kweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata walipofika walimwambia, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, wala hujali cheo cha mtu; kwa maana hutazami sura za watu; lakini katika kweli waifundisha njia ya Mungu. Je! Ni halali kumpa Kaisari kodi au siyo?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipomufikia, wakamwuliza: “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mutu wa kweli. Vilevile haushuguliki na mafikiri ya mutu lakini unafundisha kwa ukweli njia Mungu anayoamuru kufuata. Utuambie basi, Sheria inaturuhusu kulipa kodi kwa Mufalme wa Roma au hapana? Ni sherti tulipe au hapana?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta walipofika wakamwambia, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, wala hujali cheo cha mtu; kwa maana hutazami sura za watu: lakini katika kweli waifundisha njia ya Mungu. Je! ni halali kumpa Kaisari kodi au sivyo? Tumpe, tusimpe?