Mark 12:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Yesu alijua unafiki wao, akawaambia, “Mbona mnanijaribu? Nionesheni hiyo sarafu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, tulipe kodi au tusilipe?” Lakini Isa alijua unafiki wao. Akawauliza, “Mbona mnajaribu kunitega? Nileteeni hiyo dinari niione.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tumpe, tusimpe? Naye, akijua unafiki wao, akawaambia, Mbona mmenijaribu? Nileteeni dinari niione.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Yesu aliutambua unafiki wao na akawaambia, “Kwa nini mnanijaribu hivi? Mniletee moja ya sarafu ya fedha mnazotumia ili niweze kuiangalia.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini Yesu alijua unafiki wao, akawaambia, “Mbona mnanijaribu? Nionyesheni sarafu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Yesu alijua unafiki wao, akawaambia, “Mbona mnanijaribu? Nionesheni hiyo sarafu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, tulipe kodi au tusilipe?” Lakini Yesu alijua unafiki wao. Akawauliza “Mbona mnajaribu kunitega? Nileteeni hiyo dinari niione.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, tulipe kodi au tusilipe?” Lakini Isa alijua unafiki wao. Akawauliza “Mbona mnajaribu kunitega? Nileteeni hiyo dinari niione.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tumpe, tusimpe? Naye, akijua unafiki wao, akawaambia, Mbona mmenijaribu? Nileteeni dinari niione.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Yesu alijua unafiki wao, akawaambia, “Mbona mnanijaribu? Nionesheni hiyo sarafu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Iko ruhusa ya kumtolea Kaisari kodi au haiko? Tumpe au tusimpe? Kwa kuujua ujanja wao akawaambia: Mwanijaribiaje? Nileteeni shilingi, niitazame!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tumpe, tusimpe? Naye, akijua unafiki wao, akawaambia, Mbona mmenijaribu? Nileteeni dinari niione.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kwa kuwa Yesu alitambua kwamba wao ni wanafiki, akawaambia: “Sababu gani munanipima? Muniletee kikoroti kimoja cha feza hapa kusudi nikione.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nae, akijua unafiki wao, akawaambia, Mbona mmenijaribu? nileteeni dinari niione. Wakaleta.