Mark 12:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mwalimu, Mose alituagiza hivi: ‘Mtu akifa na kuacha mke bila mtoto, ndugu yake lazima amchukue huyo mama mjane, ili ampatie ndugu yake watoto.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
wakasema, “Mwalimu, Musa alituandikia kuwa kama ndugu wa mtu akifa na kumwacha mkewe bila mtoto, basi huyo mtu inampasa amwoe huyo mjane ili amzalie ndugu yake watoto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwalimu, Musa alituandikia ya kwamba ndugu ya mtu akifa, akamwacha mkewe wala hana mtoto, ndugu yake amtwae yule mkewe akampatie ndugu yake mzao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
“Mwalimu, Musa alituandikia kwamba ikiwa kaka wa mtu atafariki na kumwacha mke asiye na watoto, Basi yule kaka lazima aoe mke yule wa nduguye na kuzaa naye watoto kwa ajili ya kaka yake aliyefariki.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Mwalimu, Mose alituagiza hivi: Mtu akifa na kuacha mke bila mtoto, ndugu yake lazima amchukue huyo mama mjane amzalie watoto ndugu yake marehemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mwalimu, Mose alituagiza hivi: ‘Mtu akifa na kuacha mke bila mtoto, ndugu yake lazima amchukue huyo mama mjane, ili ampatie ndugu yake watoto.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
wakasema, “Mwalimu, Mose alituandikia kuwa kama ndugu wa mtu akifa na kumwacha mkewe bila mtoto, basi ndugu yake atamwoa huyo mjane ili amzalie ndugu yake watoto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
wakasema, “Mwalimu, Musa alituandikia kuwa kama ndugu wa mtu akifa na kumwacha mkewe bila mtoto, basi huyo mtu inampasa amwoe huyo mjane ili amzalie ndugu yake watoto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwalimu, Musa alituandikia ya kwamba ndugu ya mtu akifa, akamwacha mkewe wala hana mtoto, ndugu yake amtwae yule mkewe akampatie ndugu yake mzao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mwalimu, Mose alituagiza hivi: ‘Mtu akifa na kuacha mke bila mtoto, ndugu yake lazima amchukue huyo mama mjane, ili ampatie ndugu yake watoto.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfunzi, Mose alituandikia kama hivi: Mtu akifiwa na mkubwa wake aliyeacha mkewe, lakini hakuacha mwana, nduguye amchukue huyo mke, amzalie mkubwa wake mwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwalimu, Musa alituandikia ya kwamba ndugu ya mtu akifa, akamwacha mkewe wala hana mtoto, ndugu yake amtwae yule mkewe akampatie ndugu yake mzao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mwalimu, Musa alituamuru: ‘Mutu akiwa na ndugu yake, naye akikufa na kuacha muke wake bila mutoto, yule ndugu yake anapaswa kumwoa yule mujane na kumuzalia ndugu yake marehemu watoto.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wakamwuliza wakinena, Mwalimu, Musa alituandikia ya kwamba ndugu ya mtu akifa, akamwacha mke wake wala hana mtoto, ndugu yake amtwae yule mke wake akampatie ndugu yake mzao.