Mark 12:20 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, kulikuwa na ndugu saba. Wa kwanza alioa, akafa bila kuacha mtoto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi kulikuwa na ndugu saba. Yule wa kwanza akaoa mke, naye akafa bila kuacha mtoto yeyote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi kulikuwa na ndugu saba, wa kwanza akatwaa mke, akafa, asiache mzao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Palikuwepo na ndugu wa kiume saba. Wa kwanza alioa mke, naye alikufa bila kuacha mtoto yeyote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, kulikuwa na ndugu saba. Wa kwanza alioa, akafa bila kuacha mtoto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, kulikuwa na ndugu saba. Wa kwanza alioa, akafa bila kuacha mtoto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi walikuwapo ndugu saba. Yule wa kwanza akaoa na akafa pasipo kuwa na mtoto ye yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi palikuwepo ndugu saba. Yule wa kwanza akaoa mke, naye akafa pasipo kuwa na mtoto yeyote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi kulikuwa na ndugu saba, wa kwanza akatwaa mke, akafa, asiache mzao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, kulikuwa na ndugu saba. Wa kwanza alioa, akafa bila kuacha mtoto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kulikuwa na waume saba walio ndugu. Wa kwanza akaoa mke, lakini alipokufa hakuacha mwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi kulikuwa na ndugu saba, wa kwanza akatwaa mke, akafa, asiache mzao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi kulikuwa wandugu saba. Wa kwanza alioa mwanamuke, lakini mutu yule akakufa bila kuacha mutoto.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi palikuwa na ndugu saba; wa kwanza akatwaa mke, akafa, asiache mzao.