Mark 12:28 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mmojawapo wa waalimu wa sheria alifika, akasikia mabishano yao. Alipoona kwamba Yesu aliwajibu vyema, akajitokeza, akamwuliza, “Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwalimu mmoja wa sheria akaja, akawasikia wakijadiliana. Akiona kwamba Isa amewajibu vyema, naye akamuuliza, “Katika amri zote, ni ipi iliyo kuu?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mmojawapo wa waandishi akafika, akawasikia wakisemezana naye, akatambua ya kuwa amewajibu vema, akamwuliza, Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mwalimu wa Sheria alifika naye aliwasikia wakijadiliana. Alipoona jinsi Yesu alivyowajibu vizuri sana, alimwuliza, “Je, amri ipi ni muhimu sana kuliko zote?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mmojawapo wa walimu wa Sheria alifika, akasikia mabishano yao. Alipoona kwamba Yesu aliwajibu vyema, akajitokeza akamwuliza, “Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mmojawapo wa waalimu wa sheria alifika, akasikia mabishano yao. Alipoona kwamba Yesu aliwajibu vyema, akajitokeza, akamwuliza, “Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwalimu mmoja wa sheria akaja akawasikia wakijadiliana. Akiona kwamba Yesu amewajibu vyema, naye akamwuliza, “Katika amri zote, ni ipi iliyo kuu?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwalimu mmoja wa sheria akaja, akawasikia wakijadiliana. Akiona kwamba Isa amewajibu vyema, naye akamuuliza, “Katika amri zote, ni ipi iliyo kuu?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mmojawapo wa waandishi akafika, akawasikia wakisemezana naye, akatambua ya kuwa amewajibu vema, akamwuliza, Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mmojawapo wa waalimu wa sheria alifika, akasikia mabishano yao. Alipoona kwamba Yesu aliwajibu vyema, akajitokeza, akamwuliza, “Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akamjia mwandishi mmoja aliyewasikia, walivyobishana; naye alijua, ya kuwa amewajibu vizuri. Huyo akamwuliza: Katika maagizo yote lililo la kwanza ni lipi?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mmojawapo wa waandishi akafika, akawasikia wakisemezana naye, akatambua ya kuwa amewajibu vema, akamwuliza, Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwalimu mumoja wa Sheria alikuwa pale Yesu alipobishana na Wasadukayo. Yeye alitambua kwamba Yesu aliwajibu vizuri. Basi akamujongelea na kumwuliza: “Ni amri gani inayokuwa ya kwanza katikati ya amri zote?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mmojawapo wa waandishi akafika, amewasikia wakisemezana nae, akatambua ya kuwa amewajibu vema, akamwuliza, Katika amri zote ipi iliyo ya kwanza?