Mark 12:32 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, yule mwalimu wa sheria akamwambia, “Vyema Mwalimu! Umesema ukweli kwamba Mungu ni mmoja tu wala hakuna mwingine ila yeye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule mwalimu wa Torati akamwambia Isa, “Mwalimu, umejibu vyema kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yule mwandishi akamwambia, Hakika, Mwalimu, umesema vema ya kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na mwalimu wa Sheria akamwambia, “Umejibu vema kabisa mwalimu. Upo sahihi kusema kuwa Mungu ni mmoja, na hakuna mwingine ila yeye.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, yule mwalimu wa Sheria akamwambia, “Vyema Mwalimu! Umesema kweli kwamba Mungu ni mmoja tu wala hakuna mwingine ila yeye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, yule mwalimu wa sheria akamwambia, “Vyema Mwalimu! Umesema ukweli kwamba Mungu ni mmoja tu wala hakuna mwingine ila yeye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule mwalimu wa sheria akamwambia Yesu, “Mwalimu, umejibu vyema kwamba Mungu ni mmoja wala hakuna mwingine ila yeye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule mwalimu wa Torati akamwambia Isa, “Mwalimu, umejibu vyema kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yule mwandishi akamwambia, Hakika, Mwalimu, umesema vema ya kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, yule mwalimu wa sheria akamwambia, “Vyema Mwalimu! Umesema ukweli kwamba Mungu ni mmoja tu wala hakuna mwingine ila yeye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yule mwandishi akamwambia: Vema, mfunzi, umesema ya kweli: Mungu ni mmoja tu, hakuna mwingine ila yeye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yule mwandishi akamwambia, Hakika, Mwalimu, umesema vema ya kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule mwalimu wa Sheria akamwambia Yesu: “Ni vizuri, Ee Mwalimu! Umesema kweli kwamba Mungu ni mumoja peke yake wala hakuna mungu mwingine isipokuwa yeye.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yule mwandishi akamwambia, Hakika, mwalimu, umesema vema ya kwamba Mungu ni mmoja, wala hapana mwingine illa yeye: