Mark 12:33 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na ni lazima mtu kumpenda Mungu kwa moyo wote, kwa akili yote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani yake kama anavyojipenda mwenyewe. Jambo hili ni muhimu zaidi kuliko tambiko na sadaka zote za kuteketezwa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kumpenda Mungu kwa moyo wako wote, na kwa ufahamu wako wote, na kwa nguvu zako zote, na kumpenda jirani kama mtu anavyojipenda mwenyewe ni bora kuliko kutoa sadaka za kuteketezwa na dhabihu zote.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama nafsi yako, kwafaa kuliko sadaka nzima za kuteketezwa na dhahibu zote pia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ni muhimu zaidi kumpenda Mungu kwa moyo wako wote, kwa ufahamu wako wote, na kwa nguvu zako zote, na kumpenda jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe kuliko sadaka zote za kuteketezwa na matoleo tunayompa Mungu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Na ni lazima mtu kumpenda Mungu kwa moyo wote, kwa akili yote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani yake kama anavyojipenda mwenyewe. Jambo hili ni muhimu zaidi kuliko dhabihu na sadaka zote za kuteketezwa.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na ni lazima mtu kumpenda Mungu kwa moyo wote, kwa akili yote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani yake kama anavyojipenda mwenyewe. Jambo hili ni muhimu zaidi kuliko tambiko na sadaka zote za kuteketezwa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kumpenda Mungu kwa moyo wote na kwa akili zote na kwa nguvu zote na kumpenda jirani kama mtu anavyojipenda mwenyewe ni bora zaidi kuliko kutoa sadaka ya kuteketezwa na dhabihu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kumpenda Mungu kwa moyo wote na kwa akili zote na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama mtu anavyojipenda mwenyewe ni bora zaidi kuliko kutoa sadaka za kuteketezwa na dhabihu zote.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama nafsi yako, kwafaa kuliko sadaka nzima za kuteketezwa na dhabihu zote pia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na ni lazima mtu kumpenda Mungu kwa moyo wote, kwa akili yote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani yake kama anavyojipenda mwenyewe. Jambo hili ni muhimu zaidi kuliko tambiko na sadaka zote za kuteketezwa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena kumpenda yeye kwa moyo wote na kwa mawazo yote na kwa nguvu yote, na kumpenda mwenzio, kama unavyojipenda mwenyewe, hupita ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na vipaji vyote vya tambiko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama nafsi yako, kwafaa kuliko sadaka nzima za kuteketezwa na dhahibu zote pia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na mutu anapaswa kumupenda Mungu kwa moyo wake wote, kwa akili yake yote na kwa nguvu yake yote, naye anapaswa kumupenda mwenzake kama vile anavyojipenda mwenyewe. Mambo hayo ni bora zaidi kuliko kumutolea Mungu nyama za kuteketezwa kwa moto na sadaka zingine zote.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
na kumpenda kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote, na kwa roho yote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama nafsi yako, kwafaa kuliko kafara zote na dhabihu zote.